Home » » MAREHEMU RACHEL MWILIGWA AAGWA LEO NA KUZIKWA GOBA JIJINI DAR ES SALAAM

MAREHEMU RACHEL MWILIGWA AAGWA LEO NA KUZIKWA GOBA JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkurugenzi Mtendaji wa New Habari  Bw. Hussein Bashe akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa ulioagwa leo katika kanisa la Anglican usharika wa Ubungo na kuhudhuriwa na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, Marehemu Rachel Mwiligwa alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita na anazikwa leo huko Goba jijini Dar es salaam.
 Geneza la mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa likiwa kanisani leo wakati wa ibada ya mazishi.
 Mmoja wa wahariri wa habari za michezo New Habari Bw. Isiji akilia kwa uchungu wakati alipotoa heshima zake za mwisho kwa marehemu.
 Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga akiaga mwili wa marehemu Rachel huku akiwa ameongozana na Mwandishi wa Makamu wa Rais Boniface Makene.
 Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoa heshima zake kwa marehemu huku akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azan.
 Mwandishi Grace Hoka akilia kwa uchungu.
 Mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo Rogati Hega akitoa heshima za mwisho.
 Mwanamasumbwi Japhet Kaseba alikuwa ni miongozi mwa waombolezaji walioaga mwili wa marehemu.
 Ndugu na jamaa wa marehemu wakipita mbele ya jeneza la mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa.

Geneza la Mwili wa Marehemu Rachel Mwiligwa likiingizwa kwenye gari maalum tayari kwa kuelekea huko Goba ambako marehemu atapumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Picha zote kwa Hisani ya Full Shangwe Blog

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa