Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, atawaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri Jumatatu tarehe 7 April, 2012, saa 5 asubuhi katika viwanja vya Ikulu.
Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi waandamizi ambao watafika ikulu mapema saa 4.00 asubuhi kwa ajili ya shughuli hii.
Tunaomba majina hayo ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu mara baada ya kupata taarifa hii na mwisho wakupokea majina itakuwa saa 2.00 asubuhi ya Jumatatu, kwa sababu ifikapo saa 4.00 kamili asubuhi kila mwalika anatakiwa awe tayari ameshakaa kwenye sehemu yake aliyopangiwa.
Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika. Aidha, tunasisitiza mavazi yawe nadhifu na heshima, kwa kuwa hii ni shughuli ya Kitaifa.
Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
5 Mei, 2012
0 comments:
Post a Comment