Home » » WASANII WATAKIWA KUJIPANGA KUKABILI TEKNOLOJIA MPYA

WASANII WATAKIWA KUJIPANGA KUKABILI TEKNOLOJIA MPYA




Na
Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wameshauriwa
kujipanga katika kutumia fursa na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati
Ulimwengu ukijiandaa kuingia kwenye mfumo wa digital kutoka ule wa nalogia ifikapo mwaka 2014.
Ushauri huo umetolewa wiki
hii na Msimazi wa Vipindi vya televisheni wa Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC) Mwanga Kirahi wakati akiwasilisha mada iliyohusu Teknolojia ya kisasa
Katika Utengenezaji Filamu kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao
makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.
Alisema kuwa kuhama kutoka
mfumo wa analogia kwenda digitali kutazalisha fursa mbalimbali za kuendeleza
Sanaa nchini lakini pia ni mwanzo wa kuibuka kwa changamto nyingi ambazo kama
wasanii hawatakuwa makini basi wanaweza kupotea na kushindwa kushindana
ipasavyo.
“Mfumo wa digitali utaleta
ushindani katika kuandaa programu za televisheni, utazalisha fursa kwa kazi za
wasaniii wetu kuonekana ulimwengu mzima lakini unaweza kuwa mwanzo wa kufa kwa
ubunifu kama wasanii watategemea vifaa vya kisasa tu pasipo kuingiza ubunifu
binafsi” alisisitiza.
Katika hili aliwashauri
wasanii kutengeneza kazi zenye ubora na zisizo za kunakiri kutoka kwa wengine lakini
pia zenye ubunifu binafsi pasipo kutegemea vifaa hivi vya kisasa pekee kwani
kinyume chake ni kukataliwa kwa kazi zao na hatimaye kupwaya.
“Digital maana yake ni kazi
za Wasanii wetu kuonekana Ulimwengu mzima, sasa kama zitakuwa za kunakiri
kutoka kwa wengine na kutegemea vifaa hivi vya kisasa tu pasipo ubunifu binafsi
hatutafanikiwa. Haya pekee yanazifanya kazi zetu zisivume muda mrefu kwani
zinakuwa si original (halisi)i” alizidi kusisitiza.
Aliongeza
kuwa, wasanii
hawana budi kubadilika sasa na kuacha tabia ya wao kufanya kila kitu
kikuanzia umeneja, utunzi, uongozaji (directing), uzalishaji (producing)
na
kadhalika kwani kwa kufanya hivyo kunazifanya kazi zao kuwa na radha
moja pekee
ambayo haiwezi kudumu muda mrefu.

Wadau wengi waliofika

kupata elimu hiyo kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa waliiomba Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA) kupanga kukutana na wasanii ili kuwapa elimu juu ya
mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa