Home » » NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AFANYA ZIARA TBC

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AFANYA ZIARA TBC


Mtayarishaji
 Mwandamizi  wa Vipindi vya Televisheni wa Shirika la   Utangazaji
Tanzania (TBC), Jeff  Shellembi (kulia) akimwonesha Naibu Waziri wa
Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (kushoto)  kaseti za
kurekodi habari na vipindi mbalimbali yenye rangi nyekundu  na bluu
 iliyo chini ya kiwango ambayo hudumu kwa miezi mitatu na kuathiri
utendaji kazi wakati wa ziara ya Naibu  Waziri  huyo iliyofanyika leo
kwenye  kituo hicho cha televisheni cha TBC, Mikocheni jijini Dares
Salaam . Wa pili (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Joe
Rugarabamu na  aliyevaa kitenge ni Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa
TBC, Suzan Mungy.

 Naibu
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla (katikati)
akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya  Shirika la Utangazaji Tanzania (
TBC), Wilfred Nyachia  baada ya kumaliza ziara yake katika shirika hilo
na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa TBC, Joe  Rugarabamu.

 Fundi
Mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Ally Kagomba (kushoto)
akimwonesha Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos
Makalla, mitambo ya kurushia vipindi mbalimbali  wakati Naibu Waziri
huyo alipofanya ziara kwenye kituo cha televisheni cha TBC,leo Mikocheni
jijini Dares Salaam.


Waziri
Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla
(katikati) akizungumza na  wajumbe wa Bodi  na uongozi wa   Shirika la
Utangazaji Tanzania( TBC), mara baada kumaliza ziara yake katika shirika
hilo. PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.
********************



Na Concilia Niyibitanga na Magreth Kinabo – HABARI


NAIBU
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makalla ameitaka
Menejimenti ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) na Bodi yake
kushirikiana kwa karibu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali
ikiwa  ni pamoja na ukosefu wa vitendeakazi.


Mhe.
Makalla ameyasema hayo leo (jana) wakati akizungumza na Menejimenti ya
TBC na Bodi yake katika ofisi za kituo Televisheni ya Taifa (TBC1) cha
 Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Waziri
Makalla ameiagiza Menejimenti ya Shirika hilo kutengeneza  Mpango
Mkakati wa kukabiliana na changamoto pamoja na matatizo ya Shirika hilo
kwa kuzingatia vipaumbele na kuishauri  Bodi ya shirika kuutumia mpango
huo.


‘Tengenezeni Mpango Mkakati wa namna ya kutatua matatizo  yanayolikabili Shirika,  ili mtoe ushauri kwa Bodi’. Amesema Makalla.


Aidha,
Makalla amekiri kuwa amejionea matatizo na kuzisikia changamoto
zilizopo TBC na ameahidi kuwa Serikali iko bega kwa bega na Shirika hilo
ili kuhahikisha  kuwa matatizo hayo na changamoto hizo zinapatiwa
Ufumbuzi.


Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi   wa TBC, Bw. Joe Rugarabamu  amesema,
TBC inajitahidi kutekeleza majukumu yake ya kuhabarisha, kuelimisha na
kuburudisha jamii ya Watanzania pamoja na changamoto ya uwezo mdogo wa
kifedha, gharama kubwa za kukusanya habari, kuzihariri na kuzisambaza
kwa Watanzania wote.


Amesema
kuwa, Shirika linakabiliwa na tatizo la  uchakavu wa mitambo, gharama
kubwa za upanuzi wa usikivu nchi nzima, uendeshaji wa mitambo hasa
ukizingatia kupanda kwa gahrama za umeme na mafuta  na malipo ya
wafanyakazi zaidi ya 600.


Bw.
Rugarabamu  ameongeza kuwa, Shirika halina jengo moja la kuweka Ofisi
za Radio na Televisheni pamoja hali inayofanya  kuwa na sehemu ya Radio,
huko Barabara ya Nyerere  na Sehemu ya Televisheni, Mikocheni hivyo
kusababisha  gharama za uendeshaji kuwa kubwa.


Naye
Mtayarishaji  Vipindi  Mwandamizi wa  TBC, Bw.  Jeff Shellembi amesema,
TBC1 inakabiliwa na uhaba wa kaseti za kisasa  kwa ajili ya habari za
vipindi vya televisheni , hivyo kujikuta wakitumia kaseti zilizo chini
ya kiwango hali inayosababisha kaseti hizo kuharibu deki na kuuwa
kamera.


Bw.
Ali Kagomba ni Fundi Mitambo  wa TBC naye ameeleza kuwa, mitambo  mingi
ya Shirika hilo ya kurushia matangazo  ni chakavu na mingine ni mibovu
kabisa ikizingatia kuwa imeshapitisha muda wake wa kutumika.


“Kwa
Kitaalam na kiufundi mitambo inatakiwa kutumika kwa miaka  si zaidi ya
8, lakini mitambo yetu ina miaka  zaidi ya kumi na huathiri ubora wa
matangazo.”  Amesema Bw. Kagomba.   


Hii
ni mara ya kwanza kwa Naibu Waziri, Mhe. Makalla kufanya ziara ya
kikazi katika Shirika la TBC mara baada ya kuteuliwa kuwa Naibu wa
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa