Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Kombe La Kagame Timu Zakamilika

Kombe La Kagame Timu Zakamilika



Release No. 116

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Julai 13, 2012



TUSKER, PORTS ZAKAMILISHA TIMU KOMBE LA KAGAME

Tusker ya Kenya na Ports ya Djibouti zinawasili leo jioni kukamilisha idadi ya timu kumi na moja zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame yanayoanza kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi za kesho ni APR ya Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini itakayoanza saa 8 kamili mchana na kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico ya Burundi.
Timu zote kutoka nje ya mazoezi zimeshapangiwa viwanja vya mazoezi ambapo zitavitumia kwa mujibu wa ratiba ambayo imepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makazi ya timu hizo na viwanja vya mazoezi ni kama ifuatavyo;

Timu: Uwanja wa mazoezi: Accommodation:
APR (Rwanda) Mabibo Hostel - Marriott Hotel (Mabibo External)
AS Vita (Congo) University of Dar es Salaam - Chichi Hotel (Kinondoni)
Atletico (Burundi) Mabibo Hostel - Lunch Time Hotel (Mabibo Hostel)
Azam (Tanzania) Azam Complex - Azam Complex (Chamazi)
El Salam Wau (S. Sudan) Zanaki Sekondari - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Mafunzo (Z’bar) Kinesi - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Ports (Djibouti) Kinesi - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Simba (Tanzania) ……………………. – Vina Hotel (Mabibo Makutano)
Tusker (Kenya) Zanaki Sekondari - Rungwe Hotel (Kariakoo)
URA (Uganda) Loyola - Valentino Royal Hotel (Kariakoo)
Yanga (Tanzania) …………………. – ……………………….



RWANDA U20 YAWASILI KUIVAA NGORONGORO HEROES
Timu ya Taifa ya Rwanda ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 inatarajia kuwasili Dar es Salaam leo mchana (Julai 13 mwaka huu) kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes.
Rwanda yenye msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20 itafikia hoteli ya Sapphire. Mechi hizo zitachezwa Julai 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi na Julai 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa.
Ngorongoro Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Adolf Rishard kujiwinda kwa mechi hizo ambazo ni sehemu ya maandalizi ya kuivaa Nigeria.
Mechi dhidi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



MWANZA YATINGA FAINALI COPA COCA-COLA 2012

Mwanza imejipatia tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Julai 13 mwaka huu) kuilaza Temeke mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Mwanza walitangulia kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta kabla ya Temeke kusawazisha kwa penalti dakika ya 56 iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.
Mabao mengine ya Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa (Jumapili) yalifunga katika dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa wazu dakika ya 94 kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya 108.
Nusu fainali ya pili itachezwa leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro ambayo kwenye robo fainali iliibamiza Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma.


Boniface Wambura
Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa