Na Claudia Mayanka
Jumla ya watu 251 wameuwawa katika ajali zilizohusisha usafiri wa Bodaboda jijini Dar es salaam katika kipindi cha miezi mitatu, imefahamika.
Katika ajali hizo zaidi ya watu 1289 wamepata majeraha huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga, katika mkutano wa pamoja wa wadau wa Usalama barabarani uliofanyika jijiji Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa biashara holela inayofanywa hasa na madereva wasio na mafunzo ni chanzo cha ongezeko la ajali barabarani.
"Kwa upande mwingine wizara ya mambo ya ndani bado ina kazi kubwa ya kufanya kwenye upenyo wa biashara huria na bado kuna mwanya wa uzembe katika kusimamia kiuhakika usalama wa vyombo vya usafiri" alisema Nizar Jivani Rais wa chama cha wamiliki wa bodaboda na bajaji AAT.
Licha ya serikali kutoa maangalizo mbalimbali kwa waendesha bodaboda lakini ajali za barabarani zimeendelea kuwa wimbo wa taifa huku maisha ya wananchi yakiendelea kuteketea, na kubwa ikiwa ni ongezeko la kizazi tegemezi kutokana na wengi kuachwa wakiwa na ulemavu .

Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment