Benjamin Masese na Grace Suresh, Dar es Salaam
SAKATA la Serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi kwa kile kilichodaiwa kuandika habari za uchochezi, limechukua sura mpya, baada ya mashirika, vituo na taasisi 22 za haki za binadamu kuungana pamoja na kuitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulifungua, kabla ya kutangaza mgogoro na Serikali.
Mashirika hayo, yalikutana mjini Dar es Salaam jana, katika ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kutoa tamko hilo.
Mashirika hayo yamezitaka taasisi zote za habari, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa (UN), taasisi za kidini na umma kwa ujumla kuungana pamoja ili kuwa na kauli moja ya kupinga kitendo cha kufungiwa kwa gazeti hilo.
Akizungumza kwa niaba ya mashirika ya kijamii, Mratibu wa Mitandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Onesmo Olengurumwa, alisema wameshtushwa na kitendo cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mkangara, kuchukua uamuzi huo haraka, badala ya kufungua kesi dhidi ya mwandishi aliyeandika habari inayodaiwa kuwa ya uchochezi.
“Kwa pamoja tunaona, kufungiwa kwa gazeti hili, kumeonyesha dhahiri nia ya Serikali kuleta hofu na kuwanyamazisha wapigania haki za binadamu, vyombo vya habari na watetezi wa haki za binadamu.
“Gazeti la Mwanahalisi, limekuwa likitoa taarifa kwa umma kuhusu nani kahusika na sakata la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Stephen Ulimboka, baada ya kuona Serikali kufumbia suala hili ambapo gazeti lilifanya uchunguzi wake na kuandika habari ambayo sote tulikiri habari ile ilikidhi vigezo vyote.
Baadhi ya mashirika hayo ni LHRC, TAMWA, PAICODEO, TUFAE, MVUHA, CHAUMTA, JAWAWAVI, MFUMA, SNDF, TAS, TEF, MCT, PINGOS FORUM, TPCF, ZAFELA, MISA TAN, ZLSC, TAWLA, LEAT, SAHRINGON, Haki Madini na Jumuiya ya Elimu ya Haki za Binadamu na Amani.
Alisema kitendo cha kufungiwa kwa gazeti hilo, hakiishii kuvunja uhuru wa vyombo vya habari, bali pia kinavunja haki za kupata habari kama inavyoeleza ibara ya 19 ya mkataba wa Haki za Kijamii na Kisiasa ya mwaka 1966 (ICCPR).
Alisema kitendo hicho, kinavunja haki ya Mkataba Afrika wa Haki za Binadamu ya mwaka 1981, vile vile kifungu cha 18 cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kinachotoa uhuru wa maoni, bila kikwazo cha aina yoyote.
Pamoja na mengine, mtandao huo umetoa ushauri kwa Serikali kuacha kutumia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ili kukandamiza magazeti.
Wakati huo huo, taarifa zilizolifikia MTANZANIA zilisema kuwa Jumuiya ya Mabalozi nchini jana zilikutana na kufanya kikao cha pamoja kujadili suala la Serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi, kwa kile kilichodaiwa kuandika habari za uchochezi.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment