Dar es Salaam
RAIS wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Gratian Mukoba amejibu hoja ya Rais wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete kwa kumtaka kutaja kiwango cha fedha kichopo kwaajili ya kulipa madai yao kufuatia serikali kudai kukosa kiwango cha kuwalipa nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100.
Bwana Mukoba ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano maalumu na Radio Free afrika kuhusiana na hotuba aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tananzania kuhusiana na mapokeo ya waalimu ambao wako katika mgogoro na serikali.
Amesema serikali inapaswa kuwaweka wazi kuhusiana na lini watalipwa mafao yao badala ya kuendelea kutoa sababu zinazoendelea kuwakatisha tama taaluma yao.
Kufuatia hali hiyo Bwana Mukoba amewaomba wabunge kulijadili Bungeni, kutokana na kugusa maslahi ya taifa zima.
Naye Meneja anayeshughulikia maswala ya habari wa Shirika la Haki Elimu Nyanda Shuli ambaye amesema kuwa ipo haja ya kubuni vyanzo vingine vya mapato vitakavyoisaidia kumudu kulipa madai ya walimu kwa sababu wanafunzi hawawezi kujifunza bila walimu wao kuwepo shuleni .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu Elizabeth Mussokia ameitaka serikali na CWT kukaa meza moja na walimu kutafuta suluhu la mgogoro wao unaowaathiri wanafunzi kutokana na kushindwa kumaliza mitaala.
Mussokia amesema kutokana na mazingira magumu waliyonayo walimu wamekuwa wakifanya mgomo baridi uliopelekea kuwepo kwa matokeoa mabaya ya wanafunzi na kiwango cha elimu kushuka nchini na kubainisha kuwa serikali isipende kubeza walimu kwa kuwa hawajasomea taaluma hiyo kwa muda mrefu..
Kwa mujibu wa takwimu za haki elimu walimu wa shule ya msingi nchini wanafundisha kwa wastani wa masaa mawili na dakika nne kwa siku kati ya masaa matano na dakika 12 yaliyo katika ratiba ya siku moja.
0 comments:
Post a Comment