Home » » BAWATA: SERIKALI IGEUKIE ARV’S ASILI

BAWATA: SERIKALI IGEUKIE ARV’S ASILI

na Nasra Abdallah
BARAZA la Waganga Watafiti wa Tiba Asilia nchini (BAWATA), limeitaka serikali sasa kugeukia dawa asili za kurefusha maisha (ARV’s) kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, ili kuepuka matatizo yanayojitokeza kwa kutumia dawa za kisasa.
Tamko la waganga hao linakuja ikiwa ni siku chache tangu kutolewa kwa habari inayohusu kuwapo kwa ARV’s feki nchini na kuwaletea madhara makubwa watumiaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Bawata, Dk. Abdallah Mandai, alisema hawaoni sababu za serikali kuendelea kuagiza dawa hizo kutoka nje ya nchi wakati dawa za asili zipo.
Mandai alisema dawa za asili hazina muda wa kuisha matumizi kama ilivyo kwa dawa za kisasa na wala hazileti madhara kwa mtumiaji.
Kwa mujibu wa mganga huyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu katika kituo chake ameshapokea wagonjwa wapatao 30 ambao wamedhurika na dawa za kuongeza maisha na kuongeza kuwa alipowapatia dawa yake ya kuondoa sumu, wamepona na kurudi katika hali zao za kawaida.
“Kwa kweli mimi bado sioni sababu ya serikali kung’ang’ania kuagiza dawa hizo nje ya nchi, badala yake kinachotakiwa ni kushirikiana nasi kwa karibu ili kuona tunatatua tatizo hili na sio kutudharau kama wanavyofanya sasa,” alisema.
Pia Mandai alitumia fursa hiyo kutangaza nia yake ya kuwatibu bure wale wote ambao wanajua wamepata madhara ya dawa hizo kama njia mojawapo ya kuwasaidia.
Chanzo: Tanania Daima

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa