Kwa mara nyingine tena TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION ikiongozwa na mwenyekiti Bi Rose Mwapachu, imefanikiwa kupata madaktari kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili kujitolea muda wao wa mapumziko kusaidia kupima afya za wazee wasiojiweza. Leo watapima afya za wazee kituo cha Mbagala, Yombo, Kinondoni kata ya Kisutu na Kinondoni kata ta Mkunguni.
Wazee wengi wameonekana wana matatizo yanayohitajika vipimo zaidi katika hospitali za wilaya na pengine Hospitali ya rufaa.Tushikamane Pamoja Foundation itafanya jitihada za kuhakikisha wazee wanaohitaji huduma zaidi inapatikana
Kazi ya kugawa dawa kwa wahitaji
Madaktari na wanachama wa TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION
Madaktari wakiwa kazini
0 comments:
Post a Comment