Home » » TRENI YA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA(TAZARA) ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM –MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO.

TRENI YA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA(TAZARA) ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM –MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO.




Treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),likiwa katika stesheni ya Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Majaribio iliyofanyika kutoka Dar es Salaam-Mwakanga-Kurasini-Dar jana mchana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita  Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.


Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri,akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana.Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo akiangalia eneo la Stesheni ya Mwakanga,wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yatakayofanya Safari zake Dar es Salaam-Mwakannga na Dar-Kurasini mnamo mwezi Oktoba 2012.Majaibio hayo yalifanyika jana kuanzia Dar-Mwakanga-Kurasini.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo akishuka kwenye Kichwa cha treni kitakachofanya Safari zake Dar-Mwakanga-Kurasini mapema mwezi wa kumi.Majaribio ya sehemu ya mabehewa hayo yalifanyika jana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita  Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa