Christina Gauluhanga na Oliver Oswald, Dar es Salaam
NYUMBA ya Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Bagamoyo, Michael Mlyambongo iliyopo Tegeta Nyaishozi imebainika kutumia umeme wa wizi. Kutokana na kitendo hicho, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limeanza mchakato wa kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kukata umeme.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mdhibiti Mapato wa TANESCO, David Swira, alisema baada ya kufika nyumbani kwa Mlyambongo na kufanya ukaguzi wamebaini amechezea mita ya Luku na kutumia umeme bure.
Alisema kutokana na hatua hiyo wamefanya jitihada za kuwasiliana na Mlyambongo, lakini ameshindwa kutoa ushirikiano na hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwakata umeme.
“Tumepata usumbufu kuingia katika nyumba hii kwa kuwa, tangu tulipofika saa nne asubuhi watoto wake walishindwa kutupa ushirikiano na ilipofika saa 10 jioni tulipata msaada wa mjumbe, ndipo tulipopima na kubaini kuna udanganyifu anaufanya katika matumizi ya umeme wake,” alisema Swira.
Alisema katika nyumba 172 walizokagua wamebaini nyumba nane kati ya hizo za wateja wao wamechezea mita, ambapo asilimia kubwa ya wanaofanya udanganyifu huo ni wateja wakubwa.
“Hili linasikitisha kwa kuwa, tumebaini wateja wakubwa wengi ndiyo wanaokwepa kulipa bili za umeme kihalali, jambo hili linasababisha shirika lizidi kudidimia na sisi tutaendelea kukagua nyumba hadi nyumba,” alisema Swira.
Naye, Mdhibiti Mapato wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Didas Lwinga, alisema wamebaini uozo mkubwa kwa wateja wao ikiwa ni pamoja na kuchezea miundombinu ya umeme katika nyumba zao.
Alisema pia wamebaini ujenzi haramu wa miundombinu ya umeme, jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa maisha ya wateja wao.
“Katika hili hatuna huruma kwa kuwa tumebaini miundombinu inachezewa ovyo kwa ajili ya kuliibia shirika, nasi tumejipanga tutawakatia wote umeme iwe fundisho kwao,” alisema Lwinga.
Alitoa wito kwa wateja kuanza kujisalimisha kuepuka adhabu itakayotolewa baada ya kubainika kama wanalihujumu shirika.

Chanzo: Mtanzania

0 comments:
Post a Comment