Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ameliagiza Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC ) kuondoa sumu iliyofukiwa shimoni na kusababisha mbuzi na ng’ombe kufa katika Kijiji cha Songosongo wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Agizo hilo alilitoa mjini hapa hivi karibuni baada ya wananchi wa kijiji hicho kumweleza kuwa Kampuni ya Ndovu imechimbia uchafu wa sumu katika shimo ambalo wakati wa mvua hutiririka na kuingia katika makazi yao na mifugo yao kunywa maji hao na kufariki.
Kutokana na malalamiko hayo, alikukutana na viongozi wa kijiji, wilaya na wa TPDC na kuagiza kuondolewa kwa sumu hiyo haraka.
Alisema sumu iliyofukiwa na Kampuni ya Ndovu katika kijiji hicho zaidi ya miaka mitano iliyopita inapaswa kuondolewa kutokana na kuanza kuathiri jamii iliyozunguka eneo hilo.
“Huu ni uzembe wa hali ya juu, hatuwezi kusikia wananchi wanapiga kelele ya kutaka sumu hii iondolewe kutokana na kuleta madhara kwa mifugo lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na wahusika.
“Natoa muda wa mwezi mmoja sumu yote iliyofukiwa shimoni na kampuni ya Ndovu iwe imeondolewa hapo vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.
“Mimi nafahamu wenye kampuni wote wanaoletwa na shirika la mafuta na ndiyo wasimamizi wa kampuni hayo, kwa hiyo ni wajibu wao kuhakikisha sumu hiyo inaondolewa haraka,” alisema Simbachewene.
Alisema Oktoba 19, 2009, mbuzi na ng’ombe wa wananchi wa kijiji hicho walikufa kutokana na sumu hiyo jamii hiyo inapaswa kupatiwa fidia ya wanyama wao.
Aliuagiza uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Songosongo kuoredhesha wanyama wote waliokufa na walioathirika na sumu hiyo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya malipo ya fidia wa wafugaji hao.
Aidha, aliitaka TPDC kulipa fidia kwa wananchi hao kwa kuwachimbia kisima cha maji safi na kukiwekea uzio.
“Haiwezekani kuwazuia wananchi wasichote maji katika visima vya kampuni na kuwazibia njia kwa kuwekwa uzio, hivyo kuondoa mvutano huo ni vema kwanza wachimbiwe kisima chao na baadaye uzio uwekwe kuwatenganisha.
“Pia nawaombeni wananchi msithubutu kamwe kuharibu miundombinu ya maji kwa makusudi, nimeambiwa kwamba kuna vitendo vya wizi wa pampu na mashine za kusukumia maji kisimani.
“Mimi sikubaliani hata kidogo na vitendo vya wizi, kwa hiyo ni muhimu kudhamini na kutunza visima hivyo,” alisema Simbachawene.
Alisema Kampuni ya Pan African Energy waliwahi kuweka mashine za kusukumia maji na kutoa lita 30,000 kwa kila mkazi, lakini miundombinu iliharibiwa na wakazi wenyewe kwa kuiba mashine hizo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment