Mkuu Mizengo Pinda amesema uwekezaji binafsi katika kilimo cha kibiashara cha mashamba makubwa nchini siyo uporaji wa ardhi kwa kuwa umiliki wa rasilimali hiyo ni wa kuazima na siyo wa kuhodhi kikabaila.
Alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya siku mbili ya kasi mabadiliko katika kilimo Tanzania kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi Sept. 6, 2012).
Mhe. Pinda alisema tofauti na nchi nyingine, hata za jirani, kama Kenya, ardhi ya Tanzania ni mali ya umma na anayeihitaji kwa uwekezaji wowote hupewa kwa masharti ya kuazimwa kwa muda tu na hamilikishwi kikabaila.
“Unaweza kumilikishwa kisheria kwa masharti ya miaka 33, 66 au 99, lakini huwezi kupewa ardhi ikawa mali yako ya binafsi kwa maisha yote dumu daima na warithi wako wakawa wanao na wajukuu zako,” alisema.
Aliongeza: “Hivyo hakuna tatizo eneo likitengwa nchini kwa uwekezaji wa kilimo cha kibiashara cha mashamba makubwa, kwani ardhi ni mali ya umma na hutolewa kwa masharti ya kuikodi tu”.
Waziri Mkuu aliulizwa na waandishi wa habari kama uwekezaji katika kilimo cha mashamba makubwa siyo uporaji wa ardhi ya Watanzania.
Kuhusu uwekezaji unaotaka kufanywa na kampuni ya Marekani ya Agrisol, ambao umekuwa ukipigiwa kelele na baadhi ya watu kuwa ni uporaji wa ardhi, Mhe. Pinda alisema jambo hilo siyo kweli.
Alisema kuwa ardhi hiyo ilikuwa inakaliwa na wakimbizi kwa zaidi ya miongo mitatu na kabla ya hapo lilikuwa ni pori la Serikali, lakini baadhi ya wakimbizi walioamua kubaki Tanzania na kuomba uraia, hawataki kuhama.
Watakaokubalika kuwa raia wa Tanzania wanatakiwa wachanganyike na Watanzania wengine na siyo kubaki kwenye eneo la makambi kwa kuwa sasa siyo wakimbizi tena.
Mhe. Pinda aliuliza: “Kwa kuwa uamuzi ulikwishafanywa na Serikali kuwa waliokuwa wakimbizi lazima waondoke katika eneo hilo na sasa ardhi imeachwa wazi mnaifanyaje, mnaiacha kuwa pori?”.
Mapema katika hotuba yake mkutanoni Waziri Mkuu alisema ukuaji wa uchumi unaotokana na sekta ya kilimo hupunguza umasikini kwa haraka zaidi kuliko wa sekta nyingine kwa sababu ya mahusiano makubwa sekta nyingine.
Semina hiyo inahudhuriwa na baadhi ya Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini na wadau wengine wa sekta ya kilimo.
(mwisho)
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu.
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM
Alhamisi Sept. 6, 2012

0 comments:
Post a Comment