Home » » MUHIMBILI YAKAIDI AGIZOLA ZITO..!

MUHIMBILI YAKAIDI AGIZOLA ZITO..!


Zitto Kabwe


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeshindwa kutekeleza agizo la Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), la kutakiwa kuifunga Benki ya NMB jana.


NIPASHE jana lilifika katika eneo la Muhimbili na kukuta Benki ya NMB ikiendelea na shughuli zake za kutoa huduma kama kawaida.

Agizo la kuifunga NMB katika eneo hilo lilitolewa na kamati ya POAC juzi chini ya Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe  baada ya kubaini kuwa Muhimbili ilishindwa kutimiza agizo lililotelewa na kamati hiyo mwaka 2007/2008 la kurejesha eneo hilo mikononi mwake badala ya kuendelea kushikiliwa na mbia ambaye ni Rejent Store.

Inadaiwa kuwa mwaka 1987 Muhimbili na Regent Store, waliingia mkataba wa ukodishaji wa eneo hilo ambao ulipaswa kumalizika baada ya miaka mitano tangu kusainiwa 1992.

Akizungumza na NIPASHE jana Msemaji wa MNH, Aminieli Aligaesha, alisema hospitali inalifanyiakazi agizo hilo.
“Sawa agizo tumelipata na tunalifanyi kazi, hivyo siwezi nikasema ni lini tutakuwa tumefanya hivyo ila tupo kwenye mchakato wa kufanya hivyo,” alisema.

Kwa upande wake, Zitto alisema jana kwamba kamati yake inafuatilia utekelezaji wa agizo lake na kwamba itachukua hatua zaidi.
NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa