BAADA ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar kumuachia huru mume wa mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, aitwaye Abdullatif Fundikira (pichani) kwa kesi ya kusafirisha madawa ya kulevya iliyokuwa inamkabili, jeshi la polisi limemkamata tena na kumrudisha lupango, Ijumaa lina data kamili.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea Jumatano iliyopita katika mahakama hiyo ambapo Hakimu Riyad Shamshama alimfutia mashitaka mtuhumiwa huyo na kumuachia huru kutokana na makosa yaliyofanyika wakati wa
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea Jumatano iliyopita katika mahakama hiyo ambapo Hakimu Riyad Shamshama alimfutia mashitaka mtuhumiwa huyo na kumuachia huru kutokana na makosa yaliyofanyika wakati wa kumfungulia kesi hiyo.
Hakimu huyo aliuambia upande wa mashitaka kuwa, kama wanataka kumbadilishia mashitaka mtuhumiwa, wanatakiwa kumsubiri nje ili wamkamate na kumfungulia mashitaka upya.
Kama walivyoshauriwa, baada ya kutoka nje, polisi walimkamata Abdullatif wakati akikumbatiana na ndugu zake waliokuwa wakiamini kuwa kesi hiyo imekwisha.
Polisi walimsweka Abdullatif katika mahabusu ya mahakama hiyo ili kujiandaa kumpeleka kituoni na kisha katika ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu kwa ajili kumfungulia kesi upya.
Hali hiyo iliwafanya baadhi ya ndugu waliokuwepo mahakamani hapo kububujikwa na machozi kwani awali walishaanza kuchekelea.
chanzo:globalpublisher
0 comments:
Post a Comment