Linah, wa pili toka kushoto akiwa na wazazi wake. Tazama vazi lake kisha linganisha na vivazi vyake (angalia picha za chini)
Msanii machachari wa kike na ambaye kwa sasa anatamba na kibao kikali sana cha 'Oliver Twist - Remix', Linah Sanga amefunguka na kudai kuwa huwa anapoenda nyumbani kwa wazazi wake huwa anavaa nguo ndefu tena za kilokole zaidi ili asije kuwaudhi wazazi wake ambao wamemkuza katika maisha hayo.
Msanii huyo anapenda kuishi kizungu baada ya kuigia kwenye muziki, ingawa anadai kuwa hawezi kusahau maisha ya kidini aliyokuwa anaishi awali ambayo yalikuwa yanamfanya avae nguo za heshima tofauti na sasa.
Linah alidai kuwa tangu alipoachana na wazazi wake maisha yake yamekuwa tofauti kwani muziki kwa upande fulani umebandilisha maisha yake, kuanzia kwenye mavazi tabia na hata lifestyle.
“Napozungumza tabia haimanishi nimekuwa muhuni hapana, bali awali nilikuwa sijuani na watu maarufu lakini sasa nimekuwa nao karibu na kuna baadhi ya vitabia nimekuwa navyo lakini si kwa ubaya,” alidai.
Msanii huyo aliongeza kuwa wazazi wake wamekuwa wakimsihi sana kuvaa nguo zile zile za zamani lakini haoni kama zina nafasi kwa sasa kutokana na career aliyoichagua.
Tazama picha 8 za vivazi vya Linah, unadhani wazazi wake wapo sahihi kukerwa na hili?
Hivi karibuni wazazi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania Estelina Sanga ‘Linah’, walionesha kukerwa na mavazi ambayo mwanao huvaa akiwa jukwaani kwenye matamasha ya muziki au mtaani. Wamedai mavazi hayo yanamdharirisha na yeye na familia pia.
Tazama picha za Linah akiwa jukwaani halafu toa maoni.
0 comments:
Post a Comment