Na Amina Athumani
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Karama Nyilawila amesema kushinda kwa
Francis Cheka, katika pambano lao si kwamba aliishiwa punzi bali ni kutokana na
rafu nyingi alizofanyiwa na mpinzani wake.
Nyilawila alipigwa kwa KO raundi ya sita na Cheka katika pambano la kuwania
ubingwa wa mabara (UBO) uzito wa kg. 75, lililofanika mwishoni mwa wiki katika
Ukumbi wa PTA sabasaba, Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya pambano hilo, Nyilawila alisema faulo alizofanyiwa na
Cheka ndizo zilizomfanya asalimu amri na ameamua kukubali yaishe.
Kwa upande wake Cheka alisema siri ya yeye kushinda mapambano anayoandaliwa ni
kutokana na kufanya mazoezi mengi, hali inayomjengea kujiamini akiwa ulingoni.
Pia alisema kumpiga Nyilawila, kutamaliza minong'ono ya watu waliokuwa wakisema
mengi juu yake siku za hivi karibuni.
Cheka ambaye pia ameitaka serikali na wadau wa michezo kuwekeza udhamini katika
mchezo huo ni pambano lake la pili kupigana na Nyilawila.
Katika pambano la awali kati yake na Nyilawila lilifanyika mjini Morogoro na Cheka
kushinda kwa pointi, hivyo kuandaliwa la marudiano kumaliza ubishi kutokana na
baadhi ya watu kudai waamuzi wanampendelea bingwa huyo.
Bondia huyo kwa sasa amejipanga kupambana na mabondia kutoka nje ya nchi kwa
kuwa hapa nchini hana mpinzani.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment