Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) akimkaribisha Balozi wa mpya wa India nchini Tanzania Mhe Debnath Shaw. Balozi huyo alifika nyumbani kwa Mhe. Spika mapema jana asubuhi kwa lengo la kujitambulisha kwake na kumfikishia salamu za ushirikiano kutoka kwa Spika wa Bunge la India, Mama Meira Kumar.
Viongozi hao wakiwa na mazungumzo ya kina ambayo yalilenga kupanua wigo wa mahusiano baina ya Tanzania na India katika Nyanja za Afya (matibabu) na Elimu ya Ufundi.Prosper Minja-Bunge
0 comments:
Post a Comment