na Mwandishi wetu
VIGOGO watano
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wako nchini Marekani, Tanzania Daima Jumatano
limebaini.
Uwepo wa vigogo
hao Marekani kwa wakati mmoja, umeibua gumzo nchini hususan kwa mitandao ya
makada wa chama hicho wanaotajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015.
Vigogo hao ni
pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na mjumbe wa
Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC), Abdulhaman Kinana, ambaye amepata
kuwa kampeni meneja wa marais hao wawili.
Mwingine ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ambaye
amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa makada watakaowania urais mwaka 2015.
Wakati vigogo
hao wako nchini Marekani, kigogo mwingine wa CCM, Nape Nnauye, ambaye ni Katibu
wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, anatarajia kwenda nchini Marekani kesho.
Ingawa vigogo
hao wako Marekani kwa shughuli na sababu tofauti, mahasimu wa Waziri Membe
kisiasa wamehusisha ziara hiyo ya wazito hao na harakati za urais 2015.
Rais Kikwete
yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi. Rais na ujumbe wake uliondoka nchini
juzi na atakuwa hapo kwa siku mbili kabla ya kuelekea nchini Canada kwa ziara
nyingine rasmi ya kiserikali.
Habari zinasema
kuwa Mkapa na Kinana waliondoka nchini wakati vikao vya mchujo vya CCM
vikiendelea mjini Dodoma na wako nchini humo kwa ajili ya shughuli za taasisi
ya Mkapa Foundation na Nape anatarajia kwenda kwa shughuli zake binafsi.
Hadi sasa
hakuna kada yeyote wa CCM aliyetangaza kuwania urais, lakini mbali ya Membe,
duru za kisiasa zinawataja makada wengine wanaotaka urais kuwa ni pamoja na
mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.
Hata hivyo,
kasi ya Sumaye kuwania nafasi hiyo imepunguzwa na matokeo ya uchaguzi wa NEC,
wilayani Hanang’ ambapo aliangushwa na Dk. Mary Nagu.
Wengine ni
Samuel Sitta, Dk. Abdallah Kigoda, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha Rose Migiro
na wengine.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment