Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
SHINDANO kubwa la kumtafuta Mfalme wa Kurap Bongo lililoandaliwa na Ukumbi wa Dar Live, litaanza Jumapili hii katika ukumbi huo ulioko Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza Afrika Sana jijini Dar, Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd ambao ndiyo wamiliki wa ukumbi huo, Abdallah Mrisho, amesema mshindi atazawadiwa gari la kifahari ambalo litatangazwa hivi karibuni.
“Kuanzia kesho, vijana wajitokeze pale Dar Live kwa wingi ili kushiriki. Jumapili ya wiki hii ndiyo watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, na mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ndiyo utakuwa umeanza rasmi,” alisema Abdallah.
Aidha, mratibu wa shindano hilo, Luqman Maloto, amesema watu wajitokeze kwa wingi kwani hakuna ‘longolongo’ na majaji watakuwa ni watu wenye heshima kubwa kwenye gemu ya muziki Bongo pamoja na wananchi watakaokuwa wakihudhuria Dar Live.
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)
0 comments:
Post a Comment