na Eveline Mosi
WANANCHI
wamehamasishwa kuhudhuria maonesho ya magari yanayotarajiwa kufanyika kuanzia
Oktoba 19 hadi 21 mwaka huu katika viwanja vya Mlimani City, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Jijini
Dar es Salam, Mratibu wa maonesho hayo yanayofahamika kwa jina la Tanzania Atomative
Festival, Ally Nchahaga, alisema katika maonesho hayo, watu watajifunza mambo
mambalimbali.
Alisema
maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa mwaka wa tano mfululizo, yameanza
kukubalika na wananchi, watu watu wengi wamekuwa wakihudhuria.
“Tukiwa
tunasheherekea miaka mitano ya Atomative Festival hapa nchini, hatuna budi
kujivunia hamasa ya vijana chipukizi kujitokeza katika biashara na watumiaji wa
magari na kubadilishana ujuzi na mawazo,”alisema Nchahaga.
Aliongeza
kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk.
Abdallah Kigoda.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment