Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe
---
“ Kwa nchi za wenzetu magazeti
ya uchunguzi yanafanya kazi hizi. Kwetu magazeti yanasubiri wanasiasa
wafanye. Orodha ya Watanzania wenye akaunti Uswiss inakuja. Hoja Binafsi
kuhusu suala hili imeruhusiwa na sasa naandaa maelezo ya Hoja. Sio
suala la kutaja orodha tu bali pia hatua za kuchukua dhidi ya fedha hizo
na wenye fedha haramu zilizofichwa huko.
Zitto
Kabwe Kuna baadhi ya Watanzania wenzangu wanabeza kazi hii.
Ninachowaambia sitakata tamaa. Ninaifanya kazi hii kwa umakini mkubwa
kwa kuwa najua uhatari wake. Sikurupuki tu. Ninafanya kazi hii kwa niaba
ya Kambi ya Upinzani nikiwa Waziri kivuli wa fedha. Hii ni kazi ya
CHADEMA, sio kazi ya Zitto. Wengine wanasema mbona 'list of shame'
tulitaja majina. Ni kweli. Lakini ilituchukua wiki kadhaa kutaja majina.
Katika mkutano wa Jangwani wakati napokelewa kutoka Bungeni baada ya
kusimamishwa ubunge kufuatia hoja ya Buzwagi, tuliahidi mbele ya umma
kutaja orodha ya mafisadi. Tukataja wiki 3 baadaye mnamo Septemba 15,
2007. Tulifanya kazi ile kwa umakini sana. Tutaifanya kazi hii ya
Watanzania wenye akaunti huko uswiss kwa umakini zaidi.
Tutaweka
wazi majina ya Watanzania wenye akaunti Uswiss kwa utaratibu na
umakini. Nitataja orodha hiyo Bungeni na kamwe sitataja nje ya Bunge.
Hii ni kazi kubwa inahitaji utulivu. ” ~ Zitto Kabwe

0 comments:
Post a Comment