na
Eliwaza Emmanuel.
MWENYEKITI
wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita,
ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shindano la Miss Utalii Tanzania.
Rais
wa shindano hilo la Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo, jana
alithibitisha kufanyika uteuzi huo, akibainisha kuwa umefanyika kutokana na
mabadiliko ya mfumo wa uongozi uliofanywa katika bodi hiyo.
“Hatua
hii ni moja ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kuimarisha shindano letu na
uongozi kwa ujumla na uteuzi huu utakuwa wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia
Oktoba 22, mwaka huu,” alisema.
Chipungahelo
alisema kuteuliwa huko kwa Guninita, kumetokana na bodi hiyo kuzingatia busara,
hekima na uzoefu mkubwa alionao katika uongozi wa jamii na jumuia mbalimbali za
kitaifa na kimataifa.
Akifafanua
kuhusiana na mabadiliko hayo, Chipungahelo alisema mfumo huo mpya wa uongozi,
umefanyika kwa lengo la kuimarisha uongozi, pia ni hatua ya kulifanya shindano
la Miss Utalii Tanzania kuwa bora na kubwa ndani na nje ya nchi.
Kwa
mujibu wa rais huyo, kuwepo wa Guninita kwenye bodi hiyo kama Makamu
Mwenyekiti, sambamba na Mwenyekiti wake, Mwanahabari mkongwe, Mikidadi
Mahamoud, na wajumbe wengine wateule wa bodi hiyo, kutafungua ukurasa mpya kwa
mashindano hayo.
Chanzo:
Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment