Wasanii wa Bongo Movies wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Movies, Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movies, marehemu John Maganga leo.
Padri Evodius Miku wa Parokia ya Mwananyamala akinyunyiza maji ya baraka kwenye jeneza.
Dada wa marehemu, Janeth (katikati) akilia kwa uchungu.
Baba wa marehemu, Stephano Maganga (kulia), akiwa na uso wa huzuni.
Baba wa marehemu, Stephano Maganga (kulia), akiwa na uso wa huzuni.
ILIKUWA ni simanzi kubwa kwa wasanii nchini waliofika kwenye msiba wa msanii wa filamu, John Steve Maganga, kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho. Maganga aliaga dunia Jumamosi iliyopita na maziko yake yamefanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo watu wengi walihudhuria.
STORI NA HARUNI SANCHAWA, GPL
0 comments:
Post a Comment