Home » » Wanaojifungua njiti Muhimbili kubebeshwa kama kangarooo

Wanaojifungua njiti Muhimbili kubebeshwa kama kangarooo

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili(MNH) imeanza teknologia mpya maarufu kama Kangaroo katika kuwatunza watoto wachanga  badala ya kuwatunza katika mashine.
Teknolojia hiyo hutumika kwa mama kufungiwa mtoto kwa kitambaa maalumu kwenye tumbo lake, mfano wa mama kangaroo anavyombeba mtoto wake, ili kumsaidia kupata joto na kujihisi bado yupo na mamae kuliko kutunzwa kwenye mashine.
Hatua imekuja kufuatia takwimu kuonyesha kuwa  asilimia 17 ya watoto wachanga katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na tatizo la uzito chini ya kiwango na kumuweka katika hatari ya kupoteza maisha kwa kushindwa kuishi kulingana na mazingira ya kawaida.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwanaharakati wa watoto ambaye pia ni kiongozi wa Wodi ya Watoto Hospitali ya Muhimbili,  Rose Mathew alisema kuanza kwa huduma ya watoto kangaroo kwenye hospitali hiyo kumeokoa watoto 91 kati ya asilimia 27 ya vifo vya watoto wachanga vinavyotokea nchini Tanzania.
Alisema vifo vinavyotokea katika hospitali vinavyohusisha watoto wachanga vifo vingi ni vya  njiti kwa sababu wanatakiwa kuwa katika uangalizi mkubwa na makini tofauti na watoto waliozaliwa kawaida.
“Vifo vingi vya watoto wachanga vinavyotokea katika hospitali nyingi vinachangiwa na  ‘watoto premacture’ kwa hiyo sasa hivi Hosptali ya Taifa Muhimbili imeweza kuokoa kwa kiasi kikubwa zaidi,” alisema  Rose.
Pia alisema tokea kuanza kwa huduma ya kangaroo, MNH watoto 78 waliweza  kuwapatia matibabau na kurejea nyumbani ambapo watoto 39 waliweza kuendelea kuishi na kuendelea vizuri.
Alisema  upatikanaji wa watoto kangaroo wanaweza kupatikana kati ya watano hadi sita kwa  wiki.
Rose aliomba Serikali iweze kujitahidi  kuanzisha huduma hii katika hospital nyingine tofauti na Muhimbili ili huduma iweze kupatikana sehemu mbalimbali kwani idadi ni kubwa ya watoto kangaroo.
‘Kwa kuanzia iwe hospitali zote za rufaa’’ alisema.
Takwimu ya Shirika la Afya duniani (WHO) inaonyesha kuwa asilimia 17 ya watoto wachanga katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na uzito pungufu wa kuzaliwa ikilinganishwa na asilimia 13 ya watoto wanaozaliwa nchini Tanzania.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa