Mheshimiwa Ndugulile akisikiliza swali toka kwa Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango (hayupo pichani).
Mbunge wa Kigamboni akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na wasikilizaji wa Kipindi cha Makutano.
Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya kipindi cha Makutano, Magic FM.
Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndungulile amesema kamwe hajawahi kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali alitaka serikali imhakikishie kuwa wananchi wanashirikishwa katika hatua ya maamuzi juu ya mradi wao. Mheshimiwa Ndugulile ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu ya mradi huo katika kipindi cha Makutano, Magic FM.
Mradi huo ambao sasa ni miaka minne tangu uanze kuongelewa umezua mjadala mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni, huku Mhe Ndugulile akitolewa kwenye moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na msimamo wake juu ya mradi huo.
Alisema tatizo la serikali imekuwa haitaki kufuata sheria inayotaka ushirikishwaji wa wananchi kila hatua katika sera ya mipango miji. Pia aliongezea kusema wananchi wanataka majibu kuhusu lini mradi utaanza, wapi utaanzia, nini hatma yao hasa kuhusu fidia. Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro uliojitokeza baina yake na madiwani wa jimbo lake uliosababishwa na wao kutembelea moja vikao vya bunge kwa mualiko wa waziri wa ardhi na makazi Mhe Anna Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa kwa sasa umeisha na kila mmoja ameshajua kosa lake.
0 comments:
Post a Comment