Home » » HOT NUUUZ!!, ADAKA WATANO WAKITAKA KUVUSHA MALORI 26 KINYEMELA BANDARINI

HOT NUUUZ!!, ADAKA WATANO WAKITAKA KUVUSHA MALORI 26 KINYEMELA BANDARINI

Waziri
wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari
Bandarini jijini Dar es salaam leo jioni wakati akitoa taarifa ya
kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa  malori 26
kinyemela  bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.


Dk.
Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari
baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini
hapo.


Dk.
Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa  kutaka kutolewa kinyemela na
kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.


Mmoja
wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia)
anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo  akijitetea mbele ya
Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilo leo jinoni. Kushoto  ni Mkuu
wa Polisi Bandarini Afande FM MisilimuOfisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe


 
Mtumishi
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo
mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo
ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa  akitekeleza majukumu
yake ya kawaida katika idara yake.


Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa