Home » » Kumbukumbu ya mtangazaji wa soka pekee Afrika Mashariki na kati mpiganaji Halima Mchuka

Kumbukumbu ya mtangazaji wa soka pekee Afrika Mashariki na kati mpiganaji Halima Mchuka

Leo Jumamosi Dec 29 ni mwaka mmoja tokea mtangazaji wa kwanza wa kike kutangaza mpira katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati Halima Mchuka (pichani) kufariki dunia.

Halima Mchuka atakumbukwa kwa weledi wake wa hali ya juu katika tasnia ya utangazaji, hasa wa mpira ambapo aliweza kubuni maneno na majina mengi ambayo yanatumika hadi hii leo, mfano mkubwa ni 'mpira umeenda fyongo' akimaanisha mpira umepigwa vibaya na mchezaji.

Leo saa kumi jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa dada yake  Mwajuma Mchuka Mbezi Beach, Dar es salaam. Karibuni wote kumuenzi na kumuombea dua  shujaa huyu.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa