Home » » Naibu Waziri apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNHCR nchini

Naibu Waziri apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNHCR nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Bibi Joyce Mends-Cole, Mwakilishi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) hapa nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika leo Wizarani.
Mhe. Mahadhi akizungumza na Bibi Mends-Cole mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho.
Bibi Mends-Cole akifafanua jambo kwa Mhe. Maalim wakati wa mazungumzo yao.
Maafisa kutoka Ofisi za UNHCR hapa nchini waliofutana na Bibi Mends-Cole (hayupo pichani) alipofika Wizarani kuwasilisha Hati za Utambulisho. Kushoto ni Bi. Linmei Li  na Bi. Janet Sato-Prima.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Ali J. Mwadini na Bi. Ramla Khamis wakinukuu masuala mbalimbali wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Maalim na Bibi Mends-Cole (hawapo pichani).
Mhe. Maalim akiagana na Bibi Mends-Cole mara baada ya mazungumzo yao.


0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa