Home » » TAHADHARI DHIDI YA BARUA ZA KUGUSHI ZA KUPANGIWA VITUO VYA KAZI ZINAZOTOLEWA KWA WATAALAMU WA KADA ZA AFYA

TAHADHARI DHIDI YA BARUA ZA KUGUSHI ZA KUPANGIWA VITUO VYA KAZI ZINAZOTOLEWA KWA WATAALAMU WA KADA ZA AFYA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


  TANGAZO KWA UMMA

TAHADHARI DHIDI YA BARUA ZA KUGUSHI ZA KUPANGIWA VITUO VYA KAZI ZINAZOTOLEWA KWA WATAALAMU WA KADA ZA AFYA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamiiimekuwa ikiwapangia vituo vya kazi wahitimu wa Kada za Afya tangu mwaka 2005/2006.    Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na Matapeli wanaowarubuni na kuwaibia fedha baadhi ya waombaji wa kazi kwa lengo la kuwapangia vituo vya kazi vya Uuguzi na Wahudumu wa Afya.

Wizara inapenda kuwaarifu wananchi hususan wahitimu wa Kada mbalimbli za Afya kuwa:-

1.     Kwa mwaka 2012/2013 Wizara bado haijapata Kibali cha kuwapangia Vituo vya kazi.  Kibali hicho kitakapotolewa wananchi watatangaziwa utaratibu wa jinsi ya kuomba kupitia Runinga, Magazeti, Radio na Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz).

2.   Wizara itabadili mfumo wake wa utoaji wa barua za kupangiwa vituo vya kazi ambapo kuanzia sasa waombaji hawatapewa barua za kupangiwa vituo vya kazi bali majina ya waombaji na vituo walivyopangiwa yatatolewa kupitia Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) na wahusika watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo walivyopangiwa baada ya kuona majina yao kupitia mtandao.

3.      Upangaji wa vituo vya kazi hauwagharimu fedha yoyote.  Hivyo, waombaji wote msitoe fedha yoyote kwa ajili ya ahadi kuwa utapata ajira na mnatakiwa kuwa makini na matapeli hao.


Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
03 DESEMBA, 2012

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa