Home » » MPAMBANO WA KUFUNGUA MWAKA 2013 KUFANYIKA FRIENDS CORNER MANZESE

MPAMBANO WA KUFUNGUA MWAKA 2013 KUFANYIKA FRIENDS CORNER MANZESE





DAR ES SALAAM,


 Bondi wa ngumi za kulipwa nchini
Thomas Mashali anatarajiwa kupanda ulingoni Januari 12 katika ukumbi wa
Friends Corner Manzese Jijini Dar es Salaam kutetea Ubingwa wa Afika 
Mashariki.



 Akiongea na waandishi wa habari
Mratibu wa pambano hilo Aisha mbegu alisema mashali atapambana kuzipiga
na Mkenya Bernard Mackoliech mpambano utakaokuwa wa raundi 10.



 Alisema maandalizi yamekamilika
ikiwa pia na kutumiwa tiketi kwa bondia huyo mkenya ambaye anatarajiwa
kuwasili januari nane kwa ajili ya kupima uzito na kupanda ulingoni.



 “tunataraji mpambano utakuwa
mkali wa kukata na shoka ukizingatia mashali ameweka kambi kwa muda
mrefu nje ya mkoa lakini pia Mackoliech ni bondia mahiri ambaye anasaka
rekodi ya kwenda kucheza nje ya nchi”,alisema Aisha.



 Alisema nafasi iko wazi kwa watu
wanaotaka kudhamini ili kuhakikisha mpambano huo unafanikiwa ukizingatia
ndio mpambano wa kwanza kwa mwaka 2013 na pia mashali anavutia
mashabiki wengi.



 Kwa upande wake rais wa TPBO
amesema mapambano ya utangulizi yanatarajiwa kuwa manne na mabondi
tayari wamesaini mikataba na watatangazwa hivi karibuni.



 Bondia Thomas Mashali anatetea
ubingwa huo wa Afrika mashariki na kati ambao aliupata baada ya kumpiga
Mganda Medi Sebyala Jijini Dar es salaam mpambano uliohudhuriwa na
mashabiki lukuki.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa