Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » VIONGOZI NA WANACHAMA 15 WA CHADEMA KUTIMKIA NCCR MAGEUZI KESHO

VIONGOZI NA WANACHAMA 15 WA CHADEMA KUTIMKIA NCCR MAGEUZI KESHO


VIONGOZI waandamizi wa Chama Cha Demokrasia 

na Mendeleo 
CHADEMA pamoja na wanachama 15 wa chama 

hicho wanatarajia
 kujiunga na Chama Cha NCCR Mageuzi kesho katika

 ukumbi wa 
Hotel ya Double J jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa za chama hicho zilizotumwa kwa

 njia ya ujumbe 
mfupi wa simu ya mkononi kwa wanahabari imedaiwa 

kuwa viongozi
 hao wa CHADEMA watakutana na Mjumbe wa

 Halmashauri Kuu ya 
NCCR-Mageuzi na mshauri wa mambo ya kisiasa Danda

 Juju ambaye 
atamwakilisha, mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho

 James Mbatia.
Juju ambaye tayari amewasili mkoani Mbeya kwa 

shughuli hiyo
 maalum 
anatarajia kuwapokea viongozi hao wa CHADEMA 

ikiwa ni hatua 
za awali zinazodaiwa kukisambaratisha CHADEMA.
Hivi karibuni aliyewahi kuwa Katibu wa Mkoa wa 

CHADEMA Eddo 
Makata alitangaza kujiunga na NCCR-Mageuzi 

baada ya

 kujiuzulu 
kutoka
 CHADEMA ambapo hata hivyo viongozi wa CHADEMA 

walidai kuwa 
walimtimua uongozi na uanachama.
Wimbi la mpasuko ndani ya CHADEMA limeanza kuibuka 

baada ya madai ya kutimuliwa kwa viongozi na wanachama 

wa chama

 hicho akiwemo, Makamu Mwenyekiti Baraza la 

Vijana la 

Chadema Taifa (BAVICHA)Juliana Shonza na aliyewahi 

kugombea 

Ubunge jimbo la Mbozi Mashariki Mtera Mwampamba.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa