Home » » ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU AJULIKANA.

ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU AJULIKANA.






ALIYEKUWA  AKITAPELI  WATU  MTANDAONI  KWA  JINA  LA  RAFIKIELIMU,

AJULIKANA...Ni  Mhitimu  wa  Chuo  Kikuu  Cha  Sokoine  Morogoro  (

SUA ), Mkaazi  wa  Njombe! Zawadi   Nono  Ya  Fedha  Taslimu, Shilingi
 Laki  Tano  ( Tsh.500,000/=)  Za  Kitanzania, kutolewa  kwa  mtu
atakaye  fanikishwa  kukamatwa  kwa  tapeli  hili  la  mtandaoni.





Hatimaye  yule  tapeli  sugu  wa  mtandaoni  aliyekuwa  akiwatapeli

wananchi  mbalimbali  kwa  jina  la  RafikiElimu  akiwahadaa

kuwapatia  ajira  ajulikana .





INAPOTOKA :   Mnamo  siku  ya  tarehe  11  Machi  2013, tuliripoti

kupitia  blogu  yetu  na  katika  blogu  mbalimbali  nchini  kuhusu

kuwepo  kwa  mtu  anaye  watapeli  wananchi  fedha  kwa  kutumia  jina
 la  taasisi  yetu.  Tapeli  huyu  asiye  na  hata  chembe  ya  huruma
 kwa  masikini  wenzake, aliweka  tangazo  katika  mtandao  wa  Zoom
Tanzania, mnamo  mwanzoni  mwa  mwezi  February  2013  akitangaza
nafasi  za  kazi z a  kuvolunteer  katika  mikoa  mbali mbali  ya
Tanzania  bara. 

 Baada  ya  watu  kutuma  maombi  yao, tapeli  huyo
aliyekuwa  akijitambulisha  kwa  jina  bandia  la  EMMANUEL  ALBERT
na  kwamba  yeye  ni  HR  wa  RafikiElimu,  aliwaambia  kuwa  wamepata
 nafasi, na  kuwatumia   fomu  za  kujaza  kisha kuwataka  wamtumie
shilingi  elfu Tano ( Tshs. 5,000/=)  za  kitanzania  kwa  mpesa
kwenda  namba   0763906931  (  AMBAYO  MBAYA  ZAIDI  AMEISAJILI  KWA
JINA  LA  RAFIKIELIMU )..

Baada  ya  kumtumia  pesa , tapeli  huyo  aliwatumia  barua  na
kuwaagiza  kuripoti  kazini  katika  taasisi  mbalimbali, huku  mmoja
kati  yao  akimuagiza  aje  kuripoti  katika  ofisi  zetu.





Tulibaini  juu  ya  uwepo  wa  utapeli  huu  mara  baada  ya

kutembelewa  na  mmoja  kati  ya  wahanga  wa  utapeli  huo.   Dada

huyo  aliye jitambulisha  kwa  jina  la   HAWA  MUSSA  ambaye  ni
Muhitimu  wa  Chuo  Kikuu  Cha  Dodoma  (  2012 )  aliripoti  katika
ofisi  zetu  siku  ya  tarehe  11  Machi  2013  saa  nne  kamili
asubuhi  na  kuomba  kumuona  HR . Baada  ya  kufanya  naye
mazungumzo  ndipo  tulipo  baini  kuwepo  kwa  utapeli  unao  fanyika
kwa  jina  la  taasisi  yetu. Haraka  haraka  tukaenda  kuripoti
uhalifu  huu  kwenye  kituo  kidogo  cha  polisi  cha  Chuo  Kikuu
Cha  Dar  Es salaam, na  kukabidhiwa  RB namba   UD/RB/849/2013  WIZI
KWA  NJIA  YA  MTANDAO.










Mara  baada  ya  kupata  RB  moja  kwa  moja  tulipost    taarifa   ya

 kuwatahadharisha  wananchi  juu  ya  uwepo  wa  mtu  anaye  tapeli

watu  kwa  kutumia  jina  la  taasisi  yetu,  huku  tukiwaachia
polisi  na  kazi  ya  uchunguzi  wa  tukio  hili  la  uhalifu.  Wakati
 polisi  wakiwa  bado  wanaendelea  na  uchunguzi, siku  ya  Jumatatu
ya  jana,  tarehe  11  Machi  2013  saa  sita  kamili  asubuhi,
tulipokea  simu  kutoka  kwa  mwakilishi  wetu  wa  Mwanza, Dada
HADIJA  SEJA  akiomba  tumpe  namba  za  " MR. EMMANUEL  ALBERT "  (
HR  wa  RafikiElimu   Foundation  ).. Kwa  kuwa  tayari  tulikuwa  na
taarifa  za  jina  hilo, tulimuomba  dada   Hadija  Seja  atutaarifu
kitu  gani  kimetokea. Dada  Hadija  alitupa  taarifa  ya  kusikitisha
 sana, kwamba  kuna  mtu  mmoja  aliyemtaja  kwa  jina  moja tu  la
Gerlad  kutoka  Arusha, amewasili  jijini  Mwanza  kuripoti  katika
ofisi  za  taasisi  ya  RESTLESS  DEVELOPMENT  kwa  ajili  ya  kuanza
kazi. Mtu  huyo  naye  ni  muhanga  wa  tapeli  huyu, na  baada  ya
kumtumia  tapeli  huyo  sh. elfu  tano, tapeli  alimuagiza  aende
kuripoti  jijini   Mwanza  katika  ofisi  za  RESTLESS  DEVELOPMENT (
mabazo  kimsingi  hazipo  Mwanza  ).  Can  You  imagine, huu  ni
unyama  wa  kiwango  gani, kumfanyia  masikini  mwenzako  ushenzi
kama  huo?.






Baada  ya  kupata  taarifa  hii, moja  kwa  moja  tukaamua  sisi

wenyewe  kama  taasisi  kwenda  katika  ofisi  za  VODACOM  makao

makuu  zilizopo  Mlimani  City  ili  kuweza  kumbaini  mtu  anaye
fanya  unyama  huu...





Tunashukuru  sana  Mungu, Vodacom  walitupa  ushirikiano  wa

kutosha..  Kutoka   kwenye  database  za  Vodacom, tuligundua  kwamba,

mtumiaji  wa    0763906931  anaishi  Njombe.  Namba  hii  imesajiliwa
MPESA  tarehe  02  February  2013, hakusajili  kwa  kitambulisho
chake  halisi, bali  kwa  barua  kutoka  kwa   Mwenyekiti  wa
Serikali  za  Mitaa.  Alisajili  akiwa  NJOMBE  na  alipokea  simu
nyingi  sana.  Zaidi  ya  watu  kumi  waliingia  katika  mkenge  wake
na  kumtumia  hizo  shilingi  Elfu  Tano.









Mwanzoni  alikuwa  ana toa  hela  zake  kwa  wakala  ambaye

alisajilia  namba  hii, lakini  baadaye  alisafiri  na  kwenda

tarafa  nyingine  hivyo  basi  kushindwa  kutoa  hela  kwa  sababu
namba  ameisajili  kwa  jina  ambalo  sio  lake. Hivyo  basi  ili
kuweza  kutoa  pesa  ilimbidi, ajihamishie  salio  kutoka  katika
namba  076390631  kwenda  kwenye  namba  yake  halisi  ambayo  ni
0765283703. Hapo  ndipo  tulipo  weza  kumbaini  tapeli  huyu.





Jina  la  huyu  mtu  anaitwa  HASHIM  MKANE  na  namba  yake  halisi

ni  0765283703.  Ni  mkaazi  wa  Njombe  na  amehitimu  Chuo  Kikuu

Cha  Sokoine  ( SUA ) .   Aliwahi  kuomba  nafasi  ya  uwakala  wa
RafikiElimu  katika  wilaya  ya Njombe,  mwezi  Agosti  2012.












Baada  ya  kupata  taarifa  hizi  tuliamua  kutafuta  mbinu  za

kumkamata  kirahisi,ambapo  tulimtumia  barua  pepe, jana  jioni

kisha  ujumbe  mfupi  wa  maneno  ( SMS )  tukimwambia  aje  Dar  Es
salaam  kuhudhuria  semina  ya  siku  tano  ya  mawakala  wa
RafikiElimu ( Tukamtajia  na  malipo  ). Nadhani  alistukia  kwamba
huenda  ameshajulikana, akatuma  ujumbe  mfupi  wa  maneno  uliosomeka
:





 "   Nashukuru  kwa  taarifa  hii  ingawa  nitashindwa    kuhudhuria

kwa  kuwa  taarifa   imechelewa    kufika na  ukichukulia  mimi  ni

mwajiliwa  wa  taasisi  binafsi  hivyo  kuweza  kupata  ruhusa  kwa
siku  moja    au  mbili  ilihali  tunafanya  evaluation  ya  mradi  ni
 ngumu. natumai  kuhudhuria  semina  nyingine  kama  mtaiandaa  "





















Hapa  tukajua  jamaa  ameshastukia  mchezo  na  uwezekano  wa

kumkamata  kwa  njia  hiyo  usingekuwa  rahisi. Hivyo  basi  tumeamua

kuweka    taarifa  hii  mtandaoni  pamoja  na  picha  za  mtuhumiwa
huyu, ili  kwa  yoyote  yule  atakaye  fanikisha  kukamatwa  kwa
mtuhumiwa  huyu  aweze  kupewa   zawadi  nono  ya  shilingi  Laki
Tano  za  kitanzania .  Taarifa  nyingine  zitatumwa  kwenye  magazeti
 na  televisheni  ili  iwe  rahisi  kusambaza  ujumbe  kwa  watanzania
 wengi  na  hivyo  kurahisisha  kutiwa  hatiani  kwa  dhalimu  huyu .
Tafadhali  upatapo  ujumbe  huu, wafahamishe  na  ndugu  jamaa  na
marafiki  zako  woote...





UKIMUONA  MTU  HUYU, TOA  TAARIFA  KATIKA  KITUO  CHOCHOTE  CHA

POLISI  KILICHO  KARIBU  NAWE , KISHA  WASILIANA  NASI  KWA SIMU

0782405936. NA  ENDAPO  TAARIFA  YAKO  ITASAIDIA  KUKAMATWA  KWA
TAPELI HUYU, TUTAKUPATIA   ZAWADI  YA  FEDHA  TASLIMU  ZA  KITANZANIA
SHILINGI  LAKI  TANO ( Tsh. 500,000/ =)..





(  KWA  TAMAA  YA  PESA  KIDOGO,  AMEJIDHALILISHA, AMEDHALILISHA

TAALUMA  YAKE, AMEDHALILISHA  CHUO  CHAKE, AMEWADHALILISHA  WAZAZI,

WAKE, NDUGU , JAMAA  NA  MARAFIKI  ZAKE, KWELI  WAHENGA  WALISEMA
TAMAA  ILIMPONZA  FISI  NA   MCHUMA  JANGA , HUCHUMA  NA  WA KWA


0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa