Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA akimkabidhi Zawadi maalum Dr, Mayaki kama ishara ya Kumpongeza kwa kufanya Ziara yake TFDA.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi iliyopo chini ya Umoja wa Africa New Partnership for Africa’s Development Agency (NEPAD) Dr, Ibrahim Assane Mayaki Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA alipotembelea katika Ziara yake aliyoifanya TFDA mapema leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA Bw, Hiiti Sillo.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi iliyopo chini ya Umoja wa Africa New Partnership for Africa’s Development Agency (NEPAD) Dr, Ibrahim Assane Mayaki Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA alipotembelea katika Ziara yake aliyoifanya TFDA mapema leo.
========== ============== =======
Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA imetembelewa na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi iliyopo chini ya Umoja wa Africa New Partnership for Africa’s Development Agency (NEPAD) Dr, Ibrahim Assane Mayaki ambapo amesema kuwa amefurahishwa na Utendaji kazi wa TFDA katika Udhibiti wa Chakula na Dawa.
Dr Mayaki ameisisitiza TFDA kuwa na ushirikiano wa pamoja Africa nzima ili wawe na mtazamo unaofanana ili kuweza kuboresha Bidhaa zote za Afrika kwa ujumla katika Kiwango cha Kimataifa.
“Tunataka Africa iwe na Mtazamo unaofanana ili kama bidhaa ikliwa haina kiwango cha ubora basi bidhaa hiyo ikataliwe Africa nzima,” amesema Dr Mayaki. Aidha Dr Mayaki ameonyesha kufurahishwa na Maabara ya TFDA ambapo amesema kuwa ni Maabara yenye kiwango kinacho kubalika kimataifa.
0 comments:
Post a Comment