JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)
TAMKO LA VIONGOZI WA KIISLAM JUU YA HALI YA UVUNJIFU WA AMANI NA UCHOCHEZI WA KIDINI NCHINI
LILILOSOMWA KATIKA HOTELI YA LAMADA 09/03/2013
--
Sisi
viongozi kutoka katika Jumuiya na Taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini
tumelazimika kukutana kutafakari na kujadili kwa kina hali ya uvunjifu
wa amani na kuzorota kwa mahusiano ya kidini hapa nchini. Katika siku za
karibuni tumeshuhudia hali ya uvunjifu wa amani katika maeneo
mbalimbali nchini mwetu. Na pia tumeshuhudia matamko mbali mbali kutoka
kwa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa dini na Asasi za kiraia kulaani na
kuonya juu ya hatari inayoikabili nchi yetu.

Pamoja
na kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya uvunjifu wa amani nchini kama
kadhia ya mabucha ya nguruwe mwaka 1993, mauaji ya Waislamu katika
Msikiti wa Mwembechai mwaka 1998, mauaji ya raia katika mikutano ya
kisiasa, kutekwa na kuuawa kwa waandishi wa habari na matukio mengine
mengi, lakini matukio ya hivi karibuni ya kushambuliwa viongozi wa dini
yaliyotokea Zanzibar na vurugu za kidini mkoani Geita yamelitikisa
Taifa.

Ndugu
wananchi na wanahabari, baada ya kukaa na kutafakari mwenendo wa
matukio ya uvunjifu wa amani nchini na kutafakari baadhi ya kauli na
matamko yanayotolewa na baadhi ya Viongozi wa Serikali, Jumuiya za
Kidini na Asasi za kiraia tumeona tuseme yafuatayo:

Mosi,
Kumekuwepo na matukio kadhaa ya kusikitisha katika jamii, ya baadhi ya
watu kushambuliwa, kujeruhiwa na hata wengine kuuawa. Jambo la
kusikitisha sana ni kuwa baadhi ya kauli na matamko ya baadhi ya
viongozi wa Serikali na Viongozi wa dini yanamuelekeo wa kukuza tatizo
zaidi la mfarakano wa kidini kuliko kuleta maelewano miongoni mwa
Wanadini mbalimbali, hasa Waislamu na Wakristo.

Hatudhani
kama kauli hizi zina nia njema. Imekuwa ni kawaida kila anaposhambuliwa
au kuuawa Padri baadhi ya Viongozi wa Serikali, na wale wa Kikristo,
vyombo vya habari, baadhi ya Asasi na taasisi za kiraia wamekuwa
wakiwanyooshea vidole na kuelekeza lawama zao kwa jamii ya Waislamu kuwa
wao ndiyo wahusika wa vurugu na mauaji ya viongozi wa kidini hata kabla
ya uchunguzi kufanyika na kujulikana mhusika.

Imekuwa
ni jambo jepesi kuwanyooshea vidole Waislam pasina kuwa na ushahidi,
hata pale matukio kama ya kushambulia na kuua ambayo yana hitaji
uchunguzi wa kina, bila hata kusubiri uchunguzi wa vyombo vya usalama na
Jeshi la Polisi, tayari Waislam wanalaumiwa. Hizi tuhuma za holela dhidi ya Waislam ndizo zinazopandikiza chuki kati ya Waislam na Wakiristo.

Waislam
wanahisi kuwa wao ni muhanga (victims) wa uvunjifu wa amani. Shutuma
hizi za holela zisizokuwa na ushahidi zinawafanya Waislam wahisi kuwa
hawatendewi haki, wananyanyaswa na kufanywa daraja la pili. Mathalani,

(1) Chanzo
cha mauaji yaliyofanywa na polisi Mwembechai mwaka 1998, ambapo Mkuu wa
Mkoa wa Dar-es-Salaam wa wakati huo aliwalaumu waislam kuwa
wanawakashifu wakristo. Bila hata kufanya uchunguzi haraharaka akawaomba
radhi Wakristo na kuamuru polisi kufanya uvamizi na mauaji hayo ya
Waislam.

(2) Wakati
mwingine serikali imekuwa ikitoa kauli za waziwazi za kuwahamasisha
Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni maadui zao na
maadui wa taifa lao. Januari 2001, Waziri Mkuu wa wakati huo alisema
katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa Serikal, inazo taarifa
kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na
magaidi hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli
hiyo watu watatu waliokuwa watumishi wa Muhimbili ambao ni Waislamu
akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa mbaroni na kuwekwa mahabusu.
Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lakini chuki
dhidi ya waislam ilikuwa ishapandikizwa.

(3) Tarehe
24 Agosti 2001 Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa
Khamisi Dibagula kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali kupitia jeshi la
polisi likawatangazia wananchi wote kuwa Waislamu wamepanga kuyalipua
makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na Serikali
ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na hiyo
shari ya Waislamu. Uzushi huu uliwachochea Wakristo wawachukie Waislamu
na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwakamata na kuwaadhibu. Hivi
Waislam wajihisi vipi kwa tuhuma kama hizo zisizokuwa na ushahidi? Ni
wazi mwenendo huu unawatia wasi wasi Waislam kuwa kuna agenda ya siri
dhidi yao. Pili, Waislam kama Wanadamu wengine wanapenda kuishi kwa amani na utulivu.

Hakuna
binadamu anayependa kusemwa vibaya, kuishi kwa hofu na ukosefu wa
amani. Mwenendo wa kuwalaumu waislam kuwa wanavunja amani si jambo la
kuvumilia kwani linajenga mfarakano miongoni mwa Waislam na Wakristo.
Ifike mahali basi serikali na viongozi wa Wakristo wawe na uadilifu,
pale inapofanywa jinai basi sheria ichukue mkondo wake pale
inapothibitika kuwa jinai imetendeka na mhusika kufikishwa mbele ya
sheria; na siyo tu kukimbilia kutoa hukumu kabla ya uthibitisho wa
kimahakama. Na pale Juma anapofanya jinai basi isemwe ni Juma na si
Uislam. Mathalani; Hivi karibuni baada ya kuuawa kwa Padri Evarius Mushi huko
Unguja tukio ambalo lilifuatia baada ya tukio jingine la kupigwa risasi
na kujeruhiwa, kiongozi mwingine wa Kanisa, Padri Ambros Mkenda pia
huko Unguja, Serikali kupitia Waziri wa mambo ya ndani ilitoa kauli kuwa
ni matokeo ya kazi za ugaidi, huku baadhi ya vyombo vya habari vikitoa
mwelekeo wa lawama kwa waislam na kuyahusisha mauaji hayo na Al-Shabaab,
Al-Qaeda, Boko Haram na vikundi vingine vya Kiislam vinavyohusishwa na
ugaidi. Serikali imetoa tamko hili bila hata kufanya uchunguzi kujua
sababu za kuuawa kwa kiongozi huyo wa dini na hata bila kuwajua wauaji
hao. Hii ni hatari kubwa sana. Kulikuwa na sababu gani kwa serikali
kukimbilia kusema kuwa ni tukio la Kigaidi wakati haijafanya uchunguzi?
Huku si kutoa mwelekeo wa majibu ya uchunguzi? Sasa tunaambiwa FBI
wanafanya uchunguzi. Kwani kila mauaji yanayofanyika hapa nchini ni
ugaidi? Inaonekana lengo ni kuwapaka tope Waislamu pamoja na dini yao.

Lakini
pia tunajiuliza, kwa nini serikali isubiri mpaka Padri auwawe halafu
watoe kauli hiyo ambapo wangeliweza kuvidhibiti vikundi hivyo kabla hata
huyo mtu hajauwawa, na kunusuru maisha yake ikiwa ilijua kuwa kuna
magaidi? Wangelidhibitiwa hao wahalifu tusingelalamika, maana waislam
tusingelituhumiwa. Viongozi
wa Kikiristo pia wamekuwa wakitoa shutuma kuwa Padri Mushi ameuawa na
waislam na kwamba mauaji hayo ni ya kidini. Kauli hizi za serikali na
viongozi wa Wakristo ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu.

Kauli hizi zinachochea uhasama miongoni mwa Watanzania wakiamini kuwa kuna baadhi wanaandamwa kwa sababu ya dini yao.Ikumbukwe
pia kuwa matukio ya kuuawa au kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini na
wanadini si lazima yawe yamekusudiwa kidini. Mathalani;Gazeti
la Rai la tarehe 7/11/2012 liliandika kwamba, mauaji yaProfesa Mwakyusa
yalipangwa na kuratibiwa ndani ya shirika la watawa la Peramiho mkoani
Ruvuma ambako inaelezwa ndimo walimo wahusika wakuu wa mauaji hayo
kutokana na ugomvi wa umiliki wa mgodi wa dhahabu Lukarasi ulioko
wilayani mbinga uliokuwa unamilikiwa na shirika la Benedikt la Peramiho.

Taarifa
hizo zilisema kwamba Profesa Mwakyusa alikuwa akihifadhi nyaraka za
umiliki wa mgodi huo na yalikuwepo maagizo kutoka kwa mkubwa wa Shirika
anayetajwa kwa jina la Fr. Lambert akiwaagiza Wakurugenzi walioteuliwa
kusimamia hisa za shirika hilo kwenye mgodi huo kutofanya jambo lolote
pasipo kumshirikisha Profesa Mwakyusa. Profesa Mwakyusa aliteuliwa na
Buruda (father) Edmund na Buruda Aidani wote ikioneshwa wana hisa 2000
kwenye mgodi huo wa dhahabu.

Tofauti za kimaslahi ndizo zilizosababisha kuuawa kwa Profesa Mwakyusa. Tukio
lingine la uhalifu ni lile lililotokea katika Parokia ya Mikocheni
Jimbo kuu la Dar es salaam mwaka jana Padri Audax Kaasa Paroko aliumia
kwa kuvunjika mguu baada ya kuvamiwa na majambazi, nyumbani kwake
(Mwananchi la 25/02/2013).

Mwaka
jana katika Jimbo la Iringa Mapadri wawili wa kanisa katoliki Paroko wa
Isimani Padri Angelo Burged (60) na msaidizi wake Padri Herman Myalla
(36) walishambuliwa na majambazi na kuumizwa vibaya kwa silaha zikiwamo
risasi za moto na ambapo walinusurika kufa (Mwananchi la 25/02/2013). Kuuwawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa dini zote nchini hakukuanza leo wala si kwa viongozi wa dini ya kikristo pekee.

Hivi karibuni Mashekhe pia kujeruhiwa na kuuliwa, mbona Serikali haijasema kuwa huo ni mpango wa ugaidi? Imamu
wa Msikiti wa Mwembetanga aliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi Januari
26, 2001, na katibu wa muft wa Zanzibar alimwagiwa tindikali na watu
wasiojulikana hapo Novemba 6, 2012.

Pia
Sheikh Ali Khamisi wa msikiti wa Mwakaje huko Unguja aliuawa kwa
kupigwa mapanga akiwa shambani kwake Februari 22, 2013 lakini hakutajwa
gaidi wala gaidi hajakamatwa. Serikali iwe makini isilichukulie jambo
hili upande mmoja tu kuwa hayo ni mambo ya ugaidi na ugaidi huu
ukaelekezwa kwa waislam, ni hatari.

Hivi
sasa vijana wa kiislam wanakamatwa na kutiwa ndani kwa tuhuma za
uchochezi wa kidini na kusababisha kuuwawa kwa baadhi ya viongozi wa
dini na wengine kujeruhiwa. Kamanda wa kanda maalum alisema hayo baada
ya kuwa kuna vijana wa kiislam wanne wamekamatwa jijini Dare s Salaam
katika juma lililopita.

Vyombo
vya dola vinapaswa kufanya shughuli zake kwa umakini katika
kuyafuatilia kwa ukaribu matukio hayo ili isiwe chanzo cha kulitumbukiza
Taifa letu katika vurugu za kidini. Kwa upande wetu tunaona huu ni
wakati muafaka sasa kwa serikali na jamii mbali mbali kutafuta suluhisho
la kudumu la matatizo yaliyojitokeza ili kudumisha amani na utulivu
badala ya kuleta propaganda na chuki dhidi ya jamii ya Waislam.

VURUGU ZA KIDINI MKOANI GEITA
Kwa
mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vurugu zimesababishwa na
maelekezo ya Maaskofu na Wachungaji kwa waumini wao kuchinja wanyama kwa
ajili ya kitoweo na hata kuuza mitaani. Akizungumza na gazeti la
mtazania la tarehe 11/02/2013, Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Mangochie
alisema vurugu hizo zimekuwa zikichochewa na kituo kimoja cha redio
mkoani Mwanza alisema kutokana na Mchungaji wa kanisa la FPCF kutumia
vipaza sauti kutangaza kuwa lazima wachinje na nyama kusambazwa kwenye
bucha zao. Alisema baada ya tamko hilo asubuhi yake Wakristo walichinja
ng'ombe na mbuzi katika viwanja vya makanisa yao na kuisambaza katika
bucha zilizopo soko la msufini. Ndipo waislam wakaitana kwenda kuzuia
nyama hiyo isisambae kwenye soko la msufini na kununuliwa na waislamu
wengine. Baada ya hapo ikatokea vurugu zilizopelekea kifo cha mchungaji
na waislam sita kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo pia lilisababisha uharibifu wa mali na baadhi ya watu kukamatwa. Cha
kujiuliza ni kuwa hali hii imetoka wapi na chanzo chake ni nini? Miaka
yote waislam wamekuwa ndio wachinjaji. Na hata pale viongozi wa serikali
walipotoa maelekezo kuwa Serikali inatambua waislam ndio wanaopaswa
kuchinjwa bado walitokea wachungaji na maaskofu kupinga. Je ujasiri huu
wanautoa wapi? Mbona wachochezi hawa hawakamatwi? Sisi
viongozi wa Jumuiya na Taasisi za kiislam tumesikitishwa sana na kauli
ya Mhe. Waziri Mkuu kukataa kuwatoa waislam waliokamatwa katika tukio
lile ili kujadili suluhisho la mgogoro, kwa madai ya kutokuwa na uwezo
wa kuingilia suala hilo wakati wakristo walipompa sharti Mhe. Waziri wa
mambo ya ndani alitekeleza mara moja kuwatoa wakristo wote waliokamatwa
katika tukio lile. Hali hii inachochea chuki na hisia za kibaguzi
miongoni mwa wananchi.

MADAI YA WAISLAM Kumekuwa
na juhudi za kupotosha ukweli juu ya madai ya Waislam hapa nchini.
Lakini pia kuna juhudi kubwa zinazofanywa na baadhi ya Viongozi wa
Serikali na wa dini kuwatoa Waislam kwenye madai yao ya msingi kwa
propaganda za kuvuruga amani na utulivu. Madai makuu ya Waislam
yasipotoshwe ni haya yafuatayo:

• Serikali
iweke na kutambua utaratibu wa kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ambayo
itaendeshwa na Waislamu wenyewe kama moja ya Mahakama za nchi. Mahakama
za kadhi zitaendeshwa chini ya usimamizi wa Kadhi Mkuu na Naibu Kadhi
Mkuu watakao chaguliwa na Waislamu kwa kuzingatia sifa za kielimu katika
fani ya Sheria ya Kiislamu na kutambuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano.Mashauri yote yanayohusu ndoa, talaka, mirathi, waqf, malezi ya
watoto, hibba (zawadi), wosia, biashara, bima, benki kwa mujibu wa dini
ya Kiislamu yasikilizwe katika Mahakama ya Kadhi alimradi
mhusika/wahusika ni Waislamu. Waislam wanalidai hilo na wala si kosa la
jinai na hamna ugaidi katika hilo.

itambue kuwepo kwa vyombo huru vinavyounganisha makundi mbalimbali ya
wanadini husika na vyombo hivyo viwe na nafasi sawa katika uwakilishi wa
masuala mbali mbali ya kitaifa na kimataifa. Pia kuwe na utaratibu wa
kutambua Jumuiya au Taasisi za kidini kwa nafasi sawa katika uwakilishi
wa masuala ya kidini ndani ya Serikali. Au waumini wawe huru kuwa na
taasisi itakayo wawakilisha katika masuala yao ya kitaifa.

ifute MoU kati ya Serikali na Taasisi za Kikristo na kuwafidia Waislam
kiasi sawa cha fedha na fursa nyingine mbalimbali zilizokwenda katika
Taasisi za Kikristo kupitia MoU.

• Endapo
MoU baina ya Serikali na Wakristo itaendelea, Serikali iwalipe fidia
Waislam kwa kiasi sawa cha fedha na fursa yingine zilizokwenda katika
Taasisi za Kikristo kupitia MoU pamoja na kuwekwa MoU baina ya serikali
na Waislam.

ichukue hatua za haraka kutatua matatizo ya kudhulumiwa kwa wanafunzi
Baraza la Mitihani (NECTA). Waislam walioneshea kidole hilo mwaka jana.
Wanafunzi Waislam walipandishiwa viwango vya ufaulu wakafeli 70%.
Viliporekebishwa wakafaulu kwa kiwango kikubwa zaidi ya hapo.

Kama
mwaka jana, mwaka huu Baraza la Mitihani lilipandisha tena viwango vya
ufaulu kwa nchi nzima na kuleta janga hilo nchi nzima. Madai yetu ni
yale yale kuwa serikali iuwajibishe uongozi wa Baraza la mitihani kwani
unalipeleka Taifa letu mahala pabaya.

HITIMISHO Ndugu
wananchi na wanahabari, baada ya kukaa na kutafakari mwenendo wa
matukio ya uvunjifu wa amani nchini na kutafakari baadhi ya kauli na
matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, Jumuiya za
Kidini na Asasi za kiraia tumeazimia yafuatayo.

1. Sisi
Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini tunaungana na wapenda
amani wote kulaani kwa nguvu zote mauaji, manyanyaso na udhalilishaji
wa aina yeyote unaowalenga viongozi wa dini. Mwenendo wa mauaji yenye
kuwalenga viongozi wa dini yatalitumbukiza taifa letu kwenye janga kubwa
iwapo hatua ya kurejesha amani haitachukuliwa.

2.Tunawatahadharisha
Viongozi wa Serikali na wa dini ya Kikristo kuwa makini katika kutoa
kauli na matamko kuwashutumu Waislam kuhusika na mauaji bila ya kuwa na
ushahidi kwani kauli hizo zinaweza kulitumbukiza Taifa kwenye machafuko
ya kidini.

3. Tunavitaka
Vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa uadilifu na uzalendo na kuepuka
propaganda, chuki na uchochezi hasa inaporipoti matukio nyeti kama ya
mauaji ili kuepusha Taifa letu kuingia katika vurugu za kidini na
kuvuruga amani iliyopo nchini.

4. Tunaiomba
serikali kuacha kamata kamata dhidi ya Waislam kwa kisingizio cha
uchochezi wa kidini. Vyombo vya dola vinatakiwa kufanya kazi zao kwa
weledi, umakini na uadilifu katika kubaini wahalifu ili kuepusha
kuwadhuru wasiohusika.

5. Tunaunga
mkono kauli ya Raisi Kikwete ya kuwepo kwa mjadala baina ya Wanadini
mbalimbali ili kuzungumza na kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali
yanayochochea migogoro ya kidini hapa nchini.

6. Kimsingi
katika nchi hii hakuna mgogoro kati ya Waislam na Wakristo kwani
tunaishi pamoja kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii.
Serikali inaweza kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani kutokana na kupuuza
na kutoshughulikia madai ya msingi ya waislam. Madai hayo ni pamoja na
tatizo la Baraza la Mitihani, Kuwepo kwa Mahakama ya kadhi, suala la
Tanzania kujiunga na OIC na kuwepo kwa MoU kati ya Serikali na Kanisa
nk.

7.Tunawashukuru
Waislamu wote kwa uvumilivu mkubwa mliouonesha katika kipindi hiki
kigumu na kamata kamata ya Waislamu, kuadhibiwa na kuonywa kwa vyombo
vya habari vya kiislam. (Radio Imaan na Gazeti la Annur).

Tunawaomba
kuendelea na Subra hiyo na kutochokozeka na kutotoka kwenye Agenda.
Aidha tunawaomba Viongozi wote mliohudhuria kuwaomba Waumini wote
kuzidisha dua na kumshitakia ALLAH (s.w) dhidi ya wale wote wanaokusudia
mabaya dhidi ya dini yetu.

0 comments:
Post a Comment