Home » » WANACHAMA SIMBA WAUONDOA UONGOZI WA RAGE MADARAKANI

WANACHAMA SIMBA WAUONDOA UONGOZI WA RAGE MADARAKANI


Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani.
Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na wanachama.

Bi Hindu, mwanachama maarufu wa Simba, naye alitoa lake la moyoni kwenye mkutano huo.

Mwanachama Salum Simba, akiushutumu uongozi  wa sasa.

Mmoja wa wanachama akitoa maoni yake dhidi ya uongozi wa sasa.

Mwanachama mwingine akimchana ‘live’ Aden Rage kuhusu sakata la Mbuyu Twite na Kelvin Yondani.

Wanachama wakitoka kwa amani baada ya kumaliza mkutano.

Askari wakiangalia suala la usalama.


 WANACHAMA wa klabu ya Simba, leo walifanya kikao cha dharura kwenye Hoteli ya Star Light Mnazi Mmoja jijini Dar na kuung’oa  uongozi wa klabu hiyo uliopo madarakani chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao.

 Wanachama hao wamekabidhi uongozi wa klabu hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Rahma Kharus ‘Malkia wa Nyuki’ na kumrudisha kiongozi aliyejiuzulu hivi karibuni, Zacharia Hans Poppe. Wanachama hao wamesema wanatarajia kuitisha mkutano mkuu na kuwachagua viongozi wapya baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu inayoendelea ili kuepusha kuivuruga timu.
SOURCE:GLOBALPUBLISHER

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa