JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI” Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
12, APRIL, 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWAVYOMBO VYA HABARI
Maofisa na Wakaguzi wa Polisi 639 wamepandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi na Magereza iliyofanya kikao chake tarehe 01/04/2013 chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh, Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Tume hiyo imewapandisha vyeo Wakaguzi wasaidizi wa Polisi (A/INSP) 314 kuwa Wakaguzi kamili (INSPECTOR), Warakibu Wasaidizi wa Polisi (ASP) 161 kuwa Warakibu wa Polisi (SP),Warakibu wa Polisi 81kuwa Warakibu waandamizi wa Polisi (SSP) na Warakibu Waandamizi wa Polisi (SSP) 80 kuwa Makamishina Wasaidizi wa Polisi (ACP).
Baadhi ya wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wakuu wa vyuo vya Polisi waliopandishwa vyeo na kuwa Makamishna Wasaidizi wa Polisi (ACP) ni pamoja na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mwanza, Iringa, Ilala, Tabora, Katavi, Arusha na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar na Kidatu.
Aidha, jumla ya maofisa wa kike 25 wamepandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali kati ya hao kuna waliopandishwa kuwa warakibu wa polisi (SP), warakibu waandamizi wa polisi (SSP) na Kamishina wasaidizi wa Polisi (ACP).
Kufuatia kupandishwa vyeo kwa Maafisa na Wakaguzi hao wa Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo na kusema kuwa, kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi kila askari anayefanya kazi vizuri ana haki ya kupandishwa cheo kutoka ngazi moja hadi nyingine na anayekosea katika utendaji wake ana haki ya kuadhibiwa. Aidha amewataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi katika kuimarisha Usalama wa raia na mali zao.
Vilevile, napenda kuwajulisha kwamba, Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa matukio kadhaa yaliyotokea hapa nchini, likiwemo tukio la kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, bwana Absalom Kibanda, pamoja na matukio mengine ya uchochezi wa kisiasa na kidini.
Wakati mchakato huo wa upelelezi ukiendelea, Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa na subira na kuendelea kutoa ushirikiano wa taarifa zitakazowezesha timu ya wapelelezi kufanikisha upelelezi wa matukio hayo na watuhumiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).

0 comments:
Post a Comment