Na Hussein Makame -Maelezo
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa mara ya pili
Mhandisi Bonaventure Baya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na
Msimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC) .
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Tutubi Mangazeni,
Mhandisi Baya atatumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitano.
Pamoja na kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC,Mhandisi Baya pia ni Rais wa kwanza wa Baraza la Wahitimu
wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wataalamu wa
Mazingira nchini.
Nyadhifa nyingine
alizowahi kuzishika kabla ya uteuzi huo ni pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Huduma ya Misitu
na Mjumbe wa Bodi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Aidha Mhandisi Baya amewahi
pia kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wizara ya
Kilimo na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Misitu ya Milima ya Mashariki
(TAO).
Uteuzi huo umeanza tangu
Oktoba 08 mwaka 2012 ambapo Mhandisi Baya anatarajia kutumikia cheo hicho hadi
mwezi wa kumi mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment