Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akimkabidhi mkopo wa shis milioni 4 Mkuu wa madereva wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, Mrisho Ngongo.
Picha ya pamoja
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) imeanzisha huduma mpyaya kukopesha kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa wafanyabishara wadogo nawakati kwa masharti nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mwendeshaji Mfuko huo James Washima alisema kuwa mfuko umetimiza miaka 10ambapo imeanzisha huduma hiyo ili kuweza kukuza uchumi kwa wananchi.
Washima alisema kuwa waliowekeza katika mfuko wa uwekezajiwa pamoja na UTT watachukua mikopo kwa kutumia vipande wanavyomiliki kamasehemu ya dhamana na ikiwa pamoja kuondolewa kwa gharama za kujiunga.
vipande katika mfuko huo kutarahisha kukopa na kupunguzagharama kuweza kujiunga katika uwezeshwaji wa mikopo.
Alisema kuwa waliowekeza vipande hawataweza kukopa dhamaniyote iliyowekezwa katika mfuko lengo ni kuendelea kustawisha kiuchumi kwawananchi na kuona umhimu wa uwekezaji katika mfuko huo.
Washima alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kutoasuluhisho kwa wajasiriamali wadogo ,mfuko wa kuweka na kukopa (SACCOS) namwananchi mmoja moja katika upatikanaji wa mitaji kwa kuwezesha kutekeleza miradi ya kiuchumi.
Aidha alisema kuwa wameweka mfumo ambao utaweza kurahisishakuwafikia wananchi wa vijijini kuweza kukopa hata kama hawako katika mfumo wauwekezaji wa vipande.
Alisema mikopo hiyo katika madaraja manne ya mtu mmoja moja,kupewa dhamana ya mtualiyewekeza katika mfuko huo,mkopo kwa ajili ya taasisi pamoja na mkopo wa biashara.
0 comments:
Post a Comment