Home » » JUMUIA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO (JWK), WAILILIA SERIKALI KWA KUWAPANDISHIA USHURU WA FORODHA

JUMUIA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO (JWK), WAILILIA SERIKALI KWA KUWAPANDISHIA USHURU WA FORODHA

 Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo, Mary Kituli akihutubia katika mkutano wa dharura wa jumuia hiyo ulioitishwa na kuwajhumuisha wanajumuia hiyo kujadili mambo mbalimbali ya kupandishiwa ushuru na kodi ya taka.
 Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo, Mary Kituli akihutubia katika mkutano wa dharura wa jumuia hiyo ulioitishwa na kuwajumuisha wanajumuia hiyo kujadili mambo mbalimbali ya kupandishiwa ushuru na kodi ya taka. Wengine ni viongozi mbalimbali wa JWK.
 Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Mathias Makoi (mwenye kipaza sauti akihutubia kwenye mkutano huo.





 Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo mkuu wa dharura
Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Mathias Makoi (mwenye kipaza sauti akihutubia kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

JUMUIA ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK) wameilalamikia serikali kwa kuwapandishia ushuru wa forodha na kuwafanya kushidwa kukomboa mali zao bandarini.

Kutokana na hatua hiyo inadaiwa kwamba ongezeko la vifo vya wafanyabiashara hao vinazidi kuongezeka huku wengine wakipata maradhi mbalimbali ya shinikizo ya damu na presha baada ya kushindwa kulipa gharama hizo.

Inadaiwa kuwa wafanya biashara hao wameongezewa ushuru ghafla, ma kwamba wana lipia gharama mara mbili ya gharama za awali.

Akichanganua gharama hizo, Mwenyekiti wa JWK, Mathias Makoi alisema awali makontena hayo ya mizigo, yalikuwa yakilipiwa kwa gharama za sh. milion 18 lakini sasa gharama hizo zimepandishwa  ghafla hadi kufikia sh. milio 32.

Alisema kupitia kupanda kwa gharama hizo mara mbili zaidi, wameshindwa kwenda kuitoa mizigo hiyo iliyokaa bandarini miezi miwili na nusu hadi sasa, huku wafanya biashara hao wakiwa hawana la kufanya kwani mizigo zaidi ya 400 imekwama bandarini hapo.

Alisema, "Tulikaa kikao na Waziri wa Fedha, mawakala na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini kikao hicho kilimalizika kwa vurugu na kutoelewana kwani tulipata nafasi chache za kuzungumza malalamiko yetu".

Makoi alisema kwa sasa wamedhimia kukutana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda ili kuzungumzia jambo hilo, kwani hadi sasa wameshikwa na sintofahau juu ya nani atalipia gharama za mzigo kukaa bandarini.

Alichanganua kwamba mizigo inapokaa bandarini hulipiwa kwa gharama ya dola 80 na mizigo hiyo imekaa zaidi ya mwezi mmoja hadi sasa.

Mmoja kati ya wafanyabiashara hao, Martin Masawe alisema wanaiomba TRA, irudishe mfumo wa zamani, kwani watu wameshindwa kutoa mizigo bandarini na bidhaa zinapotea katika soko hilo.

Alisema wafanya biashara wengi wamekopa benki, hivyo hadi sasa hawajui watafanya vipi marejesho yao ikiwa mizigo hiyo imekwama kutokana na gharama ya kutoa mizigo hiyo kuzidi mara mbili.

Kufuatia kukwama kwa mizigo hiyo inadaiwa kwamba ndio kulikosababisha kifo cha mfanyabiashara aliyetambulika kwa jina mmoja, Wanyama aliyejitupa kutoka ghorifani, Mei 3 mwaka huu.

 
Mbali na Wanyama pia wafanyabiasha wengine waliodaiwa kufariki kutoka na maradhi ya presha ni pamoja na Mama Lyimo na Kavishe.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa