Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho
(katikati)
akizungumza wakati kufungua warsha siku moja ya
mapitio na
uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na
Huduma za Afya ya uzazi,
maadili na mahusiano ya
kingono kwa Vijana nchini ambapo warsha hiyo
imeshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo AMREF,
UNICEF, Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya
Ufundi kutoka Tanzania Bara na Visiwani,
TGNP, Wizara ya
Afya na ustawi wa Jamii na
nyinginezo. Kushoto ni Abdoul Coulibaly wa
UNESCO na kulia ni Mwezeshaji wa Warsha hiyo
kutoka Chuo kishirikishi
cha Elimu cha Chuo
kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo.
Mwezeshaji
wa Warsha hiyo kutoka Chuo
kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha
Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo akitoa
mwongozo kwa washiriki wa
warsha hiyo ambapo
katika majumuisho yalioamuliwa kwenye warsha
iliyofanyika leo ya kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na
Huduma za Afya
ya uzazi, maadili na mahusiano ya
kingono kwa Vijana nchini
yatawasilishwa katika mkutano
wa Mawaziri utakaohusisha nchi 21 za
Afrika Mashariki na Kusini.
Picha juu na chini ni National Program
Officer – HIV & Sexuality
Education Mathias Herman kutoka UNESCO
akichambua mpango wa majukumu ya nchi za Afrika
Mashariki na Kusini na
kutoa ufafanuzi wa matokeo ya
utafiti wa Ripoti ya hali ya Elimu na
Huduma za Afya ya
uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa
Vijana
nchini ambapo ameongeza kuwa nchi inatakiwa
kujipanga kwa kusaidiwa na
UNESCO pamoja na
washirika kuongoza jitihada za kitaifa ambazo
zitawawezesha
washirika wakubwa ambao ni vijana kushiriki katika
mikakati
ya kitaifa itakayowasidia vijana nchini kujua mtazamo wao.
Pichani ni Washirki wakifuatilia uchambuzi wa Ripoti
uliokuwa ukiwasilishwa na Mathais Herman kutoka UNESCO.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Ufundi
stadi
Bw. Raymond Benedict (kushoto) akikata kujua
kuhusu mapitio ya
Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma
za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano
ya kingono
kwa Vijana nchini, huduma zinazotolewa na serikali
na nini
hatma na vijana wameelewa kwa kiwango gani.
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya
siku moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO
nchini wakichangia maoni
yao.Pichani juu Katikati ni
Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa
Mataifa
(YUNA) Lwidiko Edward akiwakilisha vijana na kulia ni Abdoul
Coulibaly wa UNESCO
Picha juu na chini ni Washirki wakiendelea
kufuatilia
yaliyokuwa yakijiri kwenye warsha ya siku moja ya
ya mapitio
na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na
Huduma za Afya ya uzazi,
maadili na mahusiano ya
kingono kwa Vijana nchini iliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam na kufunguliwa na Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho.
Chanzo Jestina George Blog
0 comments:
Post a Comment