Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
Jumla ya madaktari sita na
wataalamu wawili, mmoja wa teknolojia na mwingine wa utawala kutoka
Misri wamewasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa tundu
ndogo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dare es
Salaam.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu ujio wa madaktari hao.
“Madaktari hawa watasaidia
kutoa tiba na kuwafundisha madaktari wetu utaalamu huu, hivyo ujio wao
utasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaotakiwa kwenda
nje ya nchi,” amesema Dk. Mwinyi.
Ameongeza kuwa madakatari hao
watakuwepo katika hospitali hiyo kuanzia Juni 10 hadi 15, mwaka huu kwa
ajili ya kutoa huduma hizo. Dk. Mwinyi aliushukuru ujio huo kwa kuwa
utasaidia kubadilishana uzoefu na teknolojia na kuboresha afya ya
Watanzania.
Kwa upande wake, Balozi wa
Misri nchini Tanzania, Hossam Omar alisema ujio wa madaktari hao ni
kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta hiyo,
ambapo watauendeleza katika maeneo mengine ya sekta hiyo na nyingine.
0 comments:
Post a Comment