WATU 13 wamepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya
Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na kosa la kufanya fujo na
kusababisha uvunjifu wa amani. Baadhi ya watuhumiwa hao ni Justine
Augustine (50), Shukuru Msuya (45), Khamisi Mohamed (42), Papa Mpaya
(41), Mcharo Makenya (36), Rashidi Selemani (31), Dafa Mponda (31),
Karimu Abdallah (22), Iddy Bakari (19), Nazira Ally (18), Rashid Yusufu
(14) na wengine wawili.
Wakisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Flora Mtarania, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Jacksoni Chidunda, alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Julai 7 mwaka huu, katika eneo la Manzese.
Mwendesha mashitaka alidai kuwa watuhumiwa walifanya vurugu katika eneo hilo, wakati huo huo wakirusha mawe sehemu mbalimbali na hivyo kusababisha usumbufu kwa watu waliokuwa karibu na maeneo hayo.
“Mnadaiwa kuwatupia mawe askari polisi na wananchi, licha ya kuelezwa kuwa ni kosa kisheria kufanya hivyo na kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema.
Hata hivyo watuhumiwa hao walikana kosa na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea, ambapo Hakimu Mtarania alidai kuwa shitaka la aina hiyo kisheria linadhaminika.
Hakimu Mtarania aliwataka washitakiwa walete wadhamini wawili wa kuaminika kila mmoja, pia wawe wameajiriwa katika taasisi yoyote inayotambulika kisheria.
Watuhumiwa walirudishwa rumande wote kwa kushindwa kukamilisha masharti yaliyoainishwa na Hakimu Mtarania na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 25, mwaka huu itakapotajwa tena.
Katika hatua nyingine, mkazi wa Mbagala Chamazi, Dar es Salaam, Juma Ahmed (34), alifikishwa katika Mahakama hiyo akikabiliwa na kosa la kuiba Sh milioni 33, mali ya Wilhelm Michael.
Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni, Kwey Rusema, Wakili wa Serikali, Mwanamina Kombakono, alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Februari na Mei, mwaka huu.
Wakili alisema kuwa mshitakiwa alikabidhiwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kununulia gari, badala yake aliamua kuzichukua na kuzifanyia mambo yake binafsi.
“Inadaiwa kuwa wewe uliaminiwa na ndugu Michael hadi kufikia hatua ya kukupa fedha hizo, lakini wewe uliamua kuzitumia kwa makubaliano tofauti, kitu ambacho ni kosa kisheria,” alisema Kombakono.
Mshtakiwa alikana kosa na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea, ambapo Hakimu Rusema alidai mshtakiwa anatakiwa aje na wadhamini wawili wa kuaminika wakiwa na hati isiyohamishika watakaoweka saini ya maandishi ya Sh. Mil 10 kila mmoja.
Hata hivyo, mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 16, mwaka huu itakapotajwa tena.
CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment