Na SUPER D
Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Iddi pili jijini Dar es salaam,katika ukumbi wa friends Corner Manzese.
Akizungumzia maandalizi ya
mpambano huo mtaalishaji wa Mpambano huo,Waziri Rosta amesema mpambano
huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na
vitongoji vyake kwani mabondia hao wanatafutana kwa muda mrefu sana na
sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo.
Aliongeza kuwa mbali na
mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na
wanaotamba hapa nchini. Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio
mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa
uzito huu wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo
wachache nchini.
Na kwa upande wa kocha
anaemnoa bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake
alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa hakuna kutokana na
mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka
siku ya mchezo nahisi mambo yatakuwa safi.
Mpambano huo utakao
sindikizwa na mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo
na Fadhili Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto
atapambana na Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya
raundi sita.
0 comments:
Post a Comment