Nape Nnauye ameamua kuvunja ukimya na kutoa utetezi wake
kuhusu kauli yake chafu iliyochapishwa na gazeti la Mtanzania
likimtuhumu kuwatusi wazee waliopendekeza uwepo wa serikali
tatu.....
Huu ni utetezi wake:
"Nimestushwa sana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu
kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!
Kwakweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani
yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri
aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori
alikuwa ni "too junior".
Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.
Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wana wajibu
mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia.
Hivyo wana wajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi
ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake
tafsiri ndio hiyo?!!!
Imenisikitisha sana!
Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity"
0 comments:
Post a Comment