MTANDAO
wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya
kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa
biashara hiyo haramu.
Hivi
karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’
amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na
hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda
kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
Wakati
Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa
ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’,
Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata
la ‘unga’.
HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia
Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti
Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa
na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata
hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au
la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada
ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, mwandishi wa habari hizi aliliingia
mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio. Kwenye
makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo
amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan.
Gazeti
la Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo
ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya
naye mazungumzo kama ifuatavyo:
Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?
Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?
Wikienda:
Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya
kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?
Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.
Wikienda: Ukweli ni upi?
Ndugu:
Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong,
kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’
anahukumiwa jela tu.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.
Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana.
Chanzo: Ijumaa Wikienda
0 comments:
Post a Comment