Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo ametembelea kambi ya kusaidia watu wenye
ulemavu wa kusikia katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam asubuhi
hii. Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa hiyo Taasisi hiyo ya Starkey Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.
Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation Bwana Bill Austin Starkey
amesema tayari huduma hiyo imeshatolewa katika hospitali ya Seliani
mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo katika miji ya Dar es Salaam na
Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Nimefurahishwa
sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya ya kuwahudumia watu na
kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia kwa mara ya
kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana katika
juhudi zetu.
Madaktari wa kitanzania walioshirikiana nao wamefanya kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey
ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na watu mashuhuri kutoka nchini
Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali kugharamia kampeni hiyo.
Picha na Ikulu
Picha na Ikulu
1 comments:
Jaman haa wau wameondoka au??? nna motto ana tatizo la kusikia natamani kama ningeweza kuonana nao
Post a Comment