Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi.Constantina Martin(kulia)
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Mpango Mpya wa
uchangiaji wa hiari mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi wasio wanachama wa
mifuko ya hifadhi ya jamii fursa ya kujiunga na mfuko huo, kushoto ni
Mkurugenzi wa Uwekezaji, mipango na Utafiti Bw. Gabriel Silayo.
Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mipango na Utafiti
kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Gabriel
Silayo(kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo yaliyofikiwa na mfuko huo
tangu kuanzishwa kwake kulia ni Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko
huo Bi.Constantina Martin. PICHA NA FRANK MVUNGI> MAELEZO.
=========== ============
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)
1.0 UTANGULIZI
PSPF ni Taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa Sheria
Namba 2 ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma ya mwaka 1999 (The
Public Service Retirement Benefits Act No.2 of 1999) sura ya 371.
Hapo awali Mfuko huu ulikuwa unahudumia watumishi wa
Serikali Kuu na Wakala wa Serikali tu. Hata hivyo, kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Msimamizi na
Mdhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (Sheria Na.8 ya mwaka 2008); fursa zaidi
zimefunguliwa ambapo sasa Mfuko wa PSPF unaweza kusajili wanachama kutoka sekta
zote iwe sekta binafsi, sekta rasmi na isiyo rasmi. Aidha mabadiliko haya yameleta uhuru kwa
mtumishi kuchagua Mfuko autakao.
Kutokana na hili PSPF inapenda kuwakaribisha wote na
inatoa taarifa rasmi kwamba sasa kila Mtanzania aliyepo ndani au nje ya nchi anaweza
kuwa mwanachama wa PSPF!
Ili kuweza kuwahudumia Watanzania wote haswa waliopo
katika sekta isiyo rasmi PSPF imeanzisha Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSPF
Supplimentary Scheme) maarufu kama PSS.
Mpango huu ulizinduliwa rasmi tarehe 07 Machi 2013 wakati
wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wadau wa PSPF, hadi kufikia tarehe 25/07/2013 mpango
huu una wanachama 730 na makusanyo ya kiasi cha shilingi milioni 135.83.
2.0 MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI
(PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME- PSS)
Mpango huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuwapatia
huduma ya hifadhi ya jamii wale wote ambao awali kutokana na matakwa ya
kisheria hawakuweza kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Vile vile mpango huu ni fursa nzuri ya kujiwekea
akiba ya ziada wanachama ambao tayari wamo katika Mifuko mbalimbali ya Hifadhi
ya Jamii.
Uanachama katika mpango huu uko wazi kwa kila Mtanzania
mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Kiasi cha mchango kwa mwezi ni shilingi 10,000/= kiwango ambacho wengi
wanaweza kukimudu kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu. Michango inaweza
kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi na hata kwa msimu kutegemeana na upatikanaji
wa kipato cha ziada. Michango hii huwekewa faida kila baada ya miezi sita.
Michango inaweza kuwasilishwa kupitia akaunti ya benki,
au kupitia Wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa na Airtel money. Mwanachama
atajaza fomu na kupewa kitambulisho na nambari ya uanachama.
Mafao yatolewayo katika mpango huu wa hiari ni kama yafuatavyo:
·
Fao la Elimu,
·
Fao la Ujasiriamali,
·
Fao la Uzeeni,
·
Fao la Ugonjwa,
·
Fao la Kifo.
Pia mwanachama anapolazimika kuchukua michango yake yote
na faida kutokana na sababu zozote zile, anaweza tena kuanza kuchangia upya
bila masharti yoyote.
Taarifa hii imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
Golden Jubilee Towers, Front Tower,
Ghorofa ya 6 -13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
S.L.P 4843, Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2120912/52, +255 222127375/76
Nukushi: +255 22 2120930,
Barua Pepe: pspf@pspf-tz.org: Tovuti: www.pspf-tz.org
0 comments:
Post a Comment