Serikali na washirika wa masuala ya
watoto nchini wamekutana kwa lengo la kutafuta mwarobaini wa kumaliza tatizo la
zaidi ya watoto 5800 wanaomba barabarani mkoani dar es salaam.
mkutano huo ni sehemu ya mkakati wa
kusaidia utimilifu wa ndoto za watoto hao katika maisha ikiwa ni pamoja na
kudhibiti mapema madhara yanayoweza kujitokeza kwa taifa kwa miaka ijayo
kufuatia ongezeko la watoto ombaomba kila wakati.
levina kikoyo ni makamu mkurugenzi wa
mradi wa tuwalee pamoja wa shirika lisilo ya kiserikali (fhi) anasema asilimia
64 ya watoto wanaomba barabarani wanatamani kwenda shuleni wakati asilimia 65
hawatamani kurudi shuleni.
kwa upande wake kaimu katibu tawala
msaidizi wa afya ofisi ya mkuu wa mkoa dar es salaam victoria bura amesema ipo
haja kwa wazazi kutotumia watoto katika suala zima la kuomba barabarani.
naye mama wa watoto sita anayeombaomba
rose james amesema ugumu wa maisha ndiyo ulichangia yeye kuombaomba licha ya
watoto wake kutamani kurudi shule.
asilimia 51 ya watanzania ni watoto na
kwamba inakadiliwa kuwa zaidi ya watoto milioni mbili wanaishi kwenye mazingira
magumu huku milioni 1.2 kati ya watoto hao wanajihusisha na kazi ngumu ikiwemo
kuomba barabarani.
0 comments:
Post a Comment